Pata taarifa kuu
DIPLOMASIA-HAKI

Mwanadiplomasia wa Senegal akamatwa na kupigwa Canada, Dakar yalaani

Mwanadiplomasia wa Senegal, nchini Canada, alijikuta akikabiliwa na hali ngumu wakati wa operesheni ya polisi na tangu wakati huo kesi hiyo imechukua sura ya kidiplomasia. Mkuu wa diplomasia ya Senegal anashutumu "kitendo cha kibaguzi na kinyama". Hapo awali, opereheni ya msako ya polisi iligeuka na kuzua sintofahamu.

Ottawa, mji mkuu wa Canada. Mwanadiplomasia wa Senegal, nchini Kanada, alijikuta matatani wakati wa operesheni ya polisi na tangu wakati huo kesi hiyo imechukua mkondo wa kidiplomasia.
Ottawa, mji mkuu wa Canada. Mwanadiplomasia wa Senegal, nchini Kanada, alijikuta matatani wakati wa operesheni ya polisi na tangu wakati huo kesi hiyo imechukua mkondo wa kidiplomasia. Michel Gagnon/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa polisi huko Gatineau, jiji ambalo matukio hayo yalifanyika, afisa wa polisi aliyekuwa ameagizwa hati aliwasilisili nyumbani kwa mwanadiplomasia wa Senegal. Ni kutokana na kukataa kwake kutoa ushirikiano ndipo afisa huyo aliwaita polisi kutekeleza kazi yake.

Pia kwa mujibu wa vikosi vya usalama nchini Canada, mwanadiplomasia huyo anayehudumu katika Ubalozi wa Senegal huko Ottawa alikuwa mkali sana, akimjeruhi na kumpiga afisa polisi mwanamke usoni na kumng'ata mwingine, jambo ambalo liliwalazimu polisi kumdhibiti mwanadiplomasia huyo wa Senegal, kwa kumkandamiza chini, kabla ya wakimshikilia nyuma ya gari lao.

Siku mbili baadaye, majibu ya Senegal hayakuchukua muda mrefu. Katika taarifa, Wizara ya Mambo ya Nje inadai kuwa imemwita Balozi mdogo wa Ubalozi wa Canada mjini Dakar, kupinga " ghasia za polisi ya Canada" mnamo Agosti 2 katika nyumba ya mwanadiplomasia wake.

Serikali ya Senegal inazungumzia "unyanyasaji wa kimwili na wa kimaadili" kwa mwanadiplomasia huyo, "mbele ya mashahidi na mbele ya watoto wake wadogo". Serikali ay Senegal inaongeza kuwa mwathirika huyo "alifungwa pingu na kupigwa kikatili, kiasi cha kushindwa kupumua, jambo lililopelekea kukimbizwa hospitalini kwa gari la wagonjwa"

Kwa upande wake, polisi wa Gatineau wanajitetea kwa kusema kuwa mwanadiplomasia huyo hakuwahi kutaja kuwa amejeruhiwa au kuwa na maumivu.imeanza uchunguzi kwa kushambuliwa kwa afisa huyo kutoak Senegal.

Kwa upande wake, Senegal inashutumu "kitendo cha ubaguzi wa rangi na kinyama" na inajianda kutoa malalamiko yake kwa kuchukua hatua yoyote inayofaa katika kesi hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.