Pata taarifa kuu
CANADA- MARIDHIANO

Canada: Hatua ya papa Francis kuomba msamaha haitoshi

Serikali ya Canada imetangaza kuwa hatua ya kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis ya kuomba msamaha kwa raia wa taifa hilo  kutokana na vitendo vya kiovu vilivyotekelezwa  katika baadhi ya shule zilizokuwa zinamilikiwa na kanisa hilo haitoshi.

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani papa Francis
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani papa Francis AFP - VINCENZO PINTO
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya serikali inakuja wakati huu ambapo papa Francis akiwasalili katika mji wa Quebec kwa mkutano na waziri mkuu wa Cananda Justin Trudeau.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki yuko nchini Canada kwa ziara ya wiki moja.

Baadhi ya wahanga wa vitendo hivyo wamekuwa wakimtaka papa kubali kuwa kulikuwepo na vitendo vya udhalillishaji wa kigono vilivyotendwa wanafunzi wa shule nchini Canada, wakitaka pia kanisa katoliki kama taasisi kuwajibikia vitendo hivyo.

Zaidi ya wanafunzi 150,000 raia wa Canada wakichukuliwa kutoka nyumbani kwao na kisha kulazimishwa kuishi shuleni kama njia moja ya kuwatenga na tamaduni pamoja na familia zao.

Trudeau, muumini wa kanisa Katoliki na ambaye babake Pierre Trudeau, alikuwa waziri mkuu wakati huo, amekuwa akitaka kanisa katoliki kuwajibishwa na yaliotokea, akiwataka kufanya zaidi.

Tayari serikali ya Canada imeomba masamaha kutokana na nafasi yake kwa yaliotekelezwa katika maeneo ya shule nchini mwake.Waziri mkuu wa zamani Stephen Harper aliomba msamaha rasimi bungeni mwaka wa 2008.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.