Pata taarifa kuu

Hali mbaya ya hewa kusini mwa Brazili: Idadi ya vifo yaongezeka hadi kufikia 56

Idadi hiyo iliongezeka siku ya Jumamosi Mei 4 nchini Brazil ambapo mafuriko yameharibu jimbo la Rio Grande do Sul kwa siku kadhaa, na kusababisha vifo vya watu 56 na wengine 67 kutoweka katika eneo hili la kusini mwa nchi ambapo mji mkuu wa mkoa wa Porto Alegre umeathirika pakubwa. Ripoti hii mpya iliwasilishwa na ulinzi wa raia wa Brazil siku ya Jumamosi.

Siku ya Ijumaa, mitaa katikati mwa jiji hilo ilivamiwa na maji kutokana na mafuriko ya kipekee ya Guaiba, mto wa kusini mwa Brazili.
Siku ya Ijumaa, mitaa katikati mwa jiji hilo ilivamiwa na maji kutokana na mafuriko ya kipekee ya Guaiba, mto wa kusini mwa Brazili. REUTERS - Diego Vara
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na gavana, jimbo la Rio Grande do Sul linakabiliwa na "janga mbaya zaidi la hali ya hewa katika historia yake" na karibu maeneo 300 yameathiriwa.

Karibu watu 25,000 walilazimika kuhama

Barabara zimekatika kutokana na mafuriko na mawasiliano yametatizika katika jimbo hili ambapo mvua inatarajiwa kunyesha angalau hadi Jumapili na mamlaka imetoa amri ya kuhama baadhi ya maeneo ya jiji la Porto Alegre.

Hesabu ya hivi punde ya mamlaka pia inaorodhesha watu 74 waliojeruhiwa na watu 24,600 ambao walilazimika kuondoka makwao, zaidi ya 8,200 kati yao ambao sasa wanapewa hifadhi katika vituo kama vile vya michezo au vituo vya kitamaduni.

Katika mmoja wao, huko Gravatai, kaskazini mwa Porto Alegre, Claudio Almiro anasema kwamba alipoondoka nyumbani kwake, "maji yalikuwa yanamfika kwenye nyonga". “Nilipoteza kila kitu,” anaeleza.

Kazi ya waokoaji ni ya kutisha, na miji mizima haifikiki, kutokana na mafuriko.

Maafa "yasiyo na kifani".

Maeneo ya makazi yalizama, barabara zimeharibiwa au madaraja yalisombwa na maji, bila kusahau kupasuka kwa mabwawa ambayo yanahatarisha hali hiyo kuwa mbaya zaidi: hasara ni kubwa. Hasara kubwa zinaripotiwa haswa katika eneo la kati la jimbo hili linalopakana na Argentina na Uruguay.

Huko Porto Alegre, mji mkuu wa kikanda wenye wakazi wapatao milioni 1.5, maafa yatakuwa "yasiyo na kifani", ameonya Gavana Eduardo Leite.

Siku ya Ijumaa, mitaa katikati mwa jiji hilo ilivamiwa na maji kutokana na mafuriko ya kipekee ya Guaiba, mto wa kusini mwa Brazili.

Mamlaka inakadiria kuwa kiwango cha Guaiba kinaweza kufikia mita 5 katika saa zijazo. Rekodi ya kihistoria, ya mwaka 1941, ni 4.71 m.

"Licha ya juhudi kubwa ya kuzuia, bwawa ambalo linazuia mto Gravatai (...) limeanza kujaa tena maji. Watu wanapaswa kuondoka katika eneo hilo", ameandika kwenye X meya wa Porto Alegre Sebastiao Melo, akimaanisha mto mwingine ambao umeanza kutiririsha maji mjini.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Porte Alegre umesitisha shughuli zake kwa muda usiojulikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.