Pata taarifa kuu

Haiti: wajumbe wa Baraza la Mpito la Rais wakula kiapo

Wajumbe tisa wa Baraza la Mpito la Rais nchini Haiti wameapishwa rasmi Alhamisi hii asubuhi huko Port-au-Prince. Sherehe ya hatua mbili ambayo inaashiria kuwekwa kwa Baraza hili na kuanza kwa kazi yake: kuunda serikali mpya na kuiondoa nchi katika hali ya usalama na uchumi.

Michel Patrick Boisvert katikati, akiwa amezungukwa na wajume wengine wanane wa Baraza la Mpito la Rais wa Haiti mnamo Aprili 25, 2024.
Michel Patrick Boisvert katikati, akiwa amezungukwa na wajume wengine wanane wa Baraza la Mpito la Rais wa Haiti mnamo Aprili 25, 2024. AP - Ramon Espinosa
Matangazo ya kibiashara

Baraza la mpito la rais lililokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu nchini Haiti, lenye jukumu la kuchukua hatamu ya nchi hiyo lililotumbukia katika mgogoro mkubwa wa kisiasa na kiusalama, limeapishwa Alhamisi hii, na kuandaa njia ya kuundwa kwa serikali ya mpito.

Katika picha,wanaonekana wajumbe tisa wa baraza hilo - wanaume wanane na mwanamke mmoja - kwenye ikulu ya rais, wakilakiwa na kelele. Wakati huo walipaswa kuhudhuria hafla ya kuwekwa kwa baraza hilo asubuhi katika Villa d'accueil, makao makuu ya waziri mkuu, ambapo mjumbe wa Baraza Régine Abraham alizungumza kwa niaba ya timu mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu. "Leo ni siku ya kwanza tu ya kazi muhimu kurejesha utulivu, nidhamu, amani na hali zinazofaa kwa uzalishaji mali katika nchi yetu inayokumbwa na jinamizi baya. Huu ni mwanzo wa jitihada ya pamoja inayolenga kurudisha taifa letu kwenye njia ya kikatiba ya kutumaini kutoa maisha bora kwa mabinti na wana wote wa Haiti.

Wakati huo ulisubiriwa kwa hamu na Wahaiti waliochoka kuishi chini ya utawala wa magenge yenye silaha, anaripoti mwandishi wetu katika Port-au-Prince, Marie André Bélange. Kwa baadhi yao, kuwekwa kwa Baraza la Mpito la Rais hufungua njia ya suluhisho la mgogoro huo. Wananchi wa Haiti wanatarajia matokeo, baraza linafahamu hili, anaeleza Frinel Joseph, mmoja wa waangalizi wa chombo hiki cha mpito. "Tuna miradi mikubwa mitano ambayo tutafanyia kazi na tutafanyia kazi haraka," amehakikishia.

Ariel Henry atangaza rasmi kujiuzulu

Wakati huo huo, Waziri Mkuu anayepingwa Ariel Henry, ambaye alitangaza mwezi Machi kwamba atajiuzulu mara tu mamlaka mpya zitakapowekwa, alirasimisha kuondoka kwa serikali yake kwa barua. “Nawashukuru raia wa Haiti kwa fursa ya kutumikia nchi yetu kwa uadilifu, hekima na heshima. Haiti itazaliwa upya,” ameandika.

Kusubiri kuundwa kwa serikali mpya, Michel Patrick Boisvert aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa mpito, kulingana na baraza la mawaziri linaloondoka. Tayari alikuwa ametia saini taarifa kadhaa rasmi kwa vyombo vya habari katika wiki za hivi karibuni, Ariel Henry baada ya kushindwa kurejea nchini mwake baada ya ziara yake nchini Kenya na kwa sasa yuko nchini Marekani. Baraza la Mpito sasa lazima lifanyie kazi kuunda serikali mpya na kumteua Waziri Mkuu.

Hatua iliyopokelewa na kuelezewa kuwa "muhimu" na Marekani kwa ajili ya kuandaa uchaguzi nchini Haiti. "Tunaungana na jumuiya ya kimataifa kuwapongeza washiriki wote wa Haiti katika mchakato wao wa kuanzisha Baraza la Mpito la Rais," amesema John Kirby, msemaji wa Ikulu ya White House. "Leo ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi huru na wa haki," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.