Pata taarifa kuu

Canada yachanganyikiwa na kukamatwa kwa mwanadiplomasia wa Senegal

Nchini Canada, siku nne baada ya polisi wake kumfanyia dhulma na kumkamata mwanadiplomasia wa Senegal, diplomasia ya Canada imeanza kujibu kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa jambo hili ambalo limechochea hasira kutoka Dakar. "Kilichotokea hakikubaliki," imelaani Wizara ya Mambo ya Nje ya Canada.

Ottawa, mji mkuu wa Canada.
Ottawa, mji mkuu wa Canada. Michel Gagnon/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Ottawa inaonekana kuiachia mzogo wa lawama polisi ya jiji la Gatineau, katika asili ya uvamizi wa mwanadiplomasia wa Senegal, na yote haya pia yanaonekana kama operesheni ya kujinasua kwa upande wa serikali ya Justin Trudeau.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Canada, inasema "ina wasiwasi mkubwa juu ya madai ya kutendewa kwa mwanadiplomasia wa Senegal na polisi wa Gatineau". Imesisitiza, ikieleza kwamba Canada inachukua majukumu yake kwa umakini sana, chini ya Mkataba wa Vienna, ambao unafafanua sheria za diplomasia.

Jumamosi, Agosti 6, jioni,  serikali ya jimbo la Quebec, ambapo kunapatikana jiji la Gatineau, ilitangaza kufunguliwa kwa uchunguzi na polisi polisi za Quebec, kufuatia uingiliaji kati wa vikosi vya usalama "ambao umezua maswali", imesema.

Kwa hakika, ni polisi wa Kanada waliokwenda, Jumanne, Agosti 2, nyumbani kwa mwanadiplomasia wa Senegal, kufuatia mwito wa baili. Maafisa walimtaja mtu "mchokozi" ambaye alimjeruhi na kumpiga afisa wa polisi usoni na kumng'ata mwingine, na kuwalazimisha kumkabili mwanadiplomasia huyo hadi chini, kabla ya kumzuilia nyuma ya gari lao.

Serikali ya Senegal ilijibu vikali na kushutumu "kitendo cha ubaguzi wa rangi na kinyama" na "unyanyasaji wa nadra".

Taifa la Canada ambalo ni mmoja wa washirika wakuu wa Senegal, limehakikisha ushirikiano mzuri kati ya wakuu wa diplomasia wa nchi hizo mbili ili kutatua suala hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.