Pata taarifa kuu
CANADA-HAKi

Kesi ya Huawei yagonga vichwa vya habari Canada

Ni sakata ya miaka mitatu ya kidiplomasia na vyombo vya sheria ambayo ilimalizika Ijumaa, Septemba 24, baada ya kuachiliwa kwa mkurugenzi wa kifedha wa kampuni kubwa ya mawasiliano ya China ya Huawei, Meng Wanzhou, ambaye aliondoka Canada alikokuwa katika kizuizi cha nyumbani, kufuatia makubaliano yaliyofikiwa na mahakama ya Marekani.

Raia wa Canada wakiwa wamebeba mabango ya kutaka Michael Spavor na Michael Kovrig waachiliwe huko Vancouver.
Raia wa Canada wakiwa wamebeba mabango ya kutaka Michael Spavor na Michael Kovrig waachiliwe huko Vancouver. REUTERS - LINDSEY WASSON
Matangazo ya kibiashara

China kwa upande wake, imewaachilia huru raia wawili wa Canada waliokamatwa na kuzuiliwa jela kwa miaka mitatu. Nchini Canada, habari hii imepokelewa vifijo na nderemo, lakini waandishi wa habari asubuhi hii wamekosoa vikali "diplomasia hii ya mateka".

Kwa mujibu wa Gazeti Le Devoir, wafungwa wawili wa Canada walioachiliwa, walikuwa "mateka wa kisiasa". Ingawa China imekuwa ikikanusha uhusiano wowote kati ya kukamatwa kwa Meng Wanzhou na raia wawaili wa Canada, hali ambayo ilitokea siku chache baadaye. "Michael wawili", kama walivyoitwa Canada, walikuwa waliathiriwa na kukamatwa kwa mkurugenzi wa Huawei, aGazeti la Le Devoir limebaini.

Gazeti la kila siku la Globe and Mail limekumbusha mazingira ambamo walikuwa wakifungwa wafungwa hao: kwa miaka mitatu kwenye chumba kidogo kilichopewa mwangaza wa saa 24 kwa siku, wakati Meng Wanzhou alikuwa akiishi katika nyumba yake ya kifahari huko Vancouver, baad aya kuachiliwa kwa dhamana.

Canada lazima "ijifunze kutoka kwa jambo hili," Gazeti la Globe And Mail limesema. Baada ya yote, China imetumia kuwazuia raia wa Canada kwa kutishia serikali ya Ottawa.

China ni nchi "hatari"

"Mambo yasiyo yenye utata huimalizika kwa vizuri," linaongeza Gazeti La Presse katika uhariri wake. "Canada ilijikuta imekwama katika mchezo wa kijiografia wa kisiasa wa nchi mbili zenye nguvu duniani. Shida ni kwamba Canada haingeweza kuipinga Marekani ambayo hapo awali ilikuwa imeomba kuikabidhi kiongozi wa China. Kwa sababu tukianza kusema hapana kwa Marekani na kuinyenyekea China, itakuwa ni vigumu kwa Canada? " Gazeti la La Presse limehoji:" Kipindi hiki kinapaswa kutukumbusha jambo moja, China ni nchi hatari ".

Kwa upande wake, Beijing imesema Jumamosi, Septemba 25 kwamba shutuma dhidi ya kiongozi wa Huawei "zimebuniwa kabisa", na ilikuwa "dhulma ya kisiasa" limesema shirika la habari la AFP, wakati kiongozi wa kampuni kubwa ya mawasiliano ya China anarudi China baada ya kurudishwa kutoka Canada na kesi iliyodumu kwa miaka kadhaa.

"Madai ya udanganyifu dhidi ya Meng Wangzhou ni ya uwongo kabisa," msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje amesema, akinukuliwa na shirika la utangazaji la serikali CCTV.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.