Pata taarifa kuu
CHINA-HAKI

China yamhukumu kifo raia wa Canada

Mahakama ya Wachina imethibitisha hukumu ya kifo dhidi ya raia wa Canada kwa biashara ya dawa za kulevya, siku moja baada ya uamuzi mwingine wa mahakama ya juu katika kesi inayomhusu mtuhumiwa wa ujasusi wa Canada.

Raia wa Canada Robert Schellenberg, aliyekamatwa kwa biashara ya dawa za kulevya nchini China mwaka 2014, alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani mwishoni mwa mwaka 2018 na kisha kifo katika Mahakama ya Rufaa mwezi Januari 2019, mwezi mmoja baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa Huawei katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Vancouver, kwa waranti uliotolewa na Marekani.
Raia wa Canada Robert Schellenberg, aliyekamatwa kwa biashara ya dawa za kulevya nchini China mwaka 2014, alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani mwishoni mwa mwaka 2018 na kisha kifo katika Mahakama ya Rufaa mwezi Januari 2019, mwezi mmoja baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa Huawei katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Vancouver, kwa waranti uliotolewa na Marekani. AP - Vincent Yu
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo unakuja wakati nchini Canada, wanasheria wa Meng Wanzhou, afisa mkuu wa kifedha wa kampuni kubwa ya mawasiliano ya Huawei, akijaribu mara ya mwisho kuzuia kupelekwa kwake nchini Marekani, ambapo anatuhumiwa kwa kukiuka kanuni za kisheria.

Raia wa Canada Robert Schellenberg, aliyekamatwa kwa biashara ya dawa za kulevya nchini China mwaka 2014, alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani mwishoni mwa mwaka 2018 na kisha kifo katika Mahakama ya Rufaa mwezi Januari 2019, mwezi mmoja baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa Huawei katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Vancouver, kwa waranti uliotolewa na Marekani.

Meng Wanzhou anatuhumiwa kudanganya taasisi ya HSBC kuhusu biashara za Huawei nchini Iran, hali ambayo ilisababisha benki hiyo kukiuka vikwazo vya kiuchumi vya Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.