Pata taarifa kuu
CHINA

Xinjiang: China yachukuwa vikwazo dhidi ya maafisa wa Marekani na Canada

China imewachukulia vikwazo maafisa wawili wa shirika llinalotetea uhuru wa dini kutoka Marekani na mbunge mmoja wa Canada kujibu vikwazo vilivyochukuliwa na Marekani na Canada kuhusu Xinjiang.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Wang Wenbin ameshika picha za wanawake wawili kutoka jamii ya Uyghur wakati akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Beijing, China Februari 23, 2021,
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Wang Wenbin ameshika picha za wanawake wawili kutoka jamii ya Uyghur wakati akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Beijing, China Februari 23, 2021, REUTERS - REUTERS TV
Matangazo ya kibiashara

Mapema wiki hii, Marekani, Umojaa wa Ulaya, Canada na Uingereza zilichukuwa vikwazo dhidi ya maafisa wa China kwa ukiukaji wa haki za binadamu huko Xinjiang.

China inapanga kuchukua hatua dhidi ya Mwenyekiti na Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Marekani ya Uhuru wa Kidini wa Kimataifa (USCIRF) Gayle Manchin na Tony Perkins, wizara ya Mambo ya nje imesema katika taarifa.

Beijing pia imeamua kumchukulia vikswazo mbunge wa Canada Michael Chong, makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya maswala ya nje na maendeleo ya kimataifa (FAAE) na kamati ndogo ya FAAE ya haki za binadamu ambaye aliwasilisha ripoti mwezi huu akihitimisha kuwa ukatili uliofanywa huko Xinjiang ni uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya halaiki.

Watu hawa ni marufuku kuingia China Bara, Hong Kong na Macau, wizara ya Mambo ya nje imesema, na makampuni ya China na raia wamekatazwa kufanya biashara nao au kufanya biashara na tume ndogo ya FAAE ya haki za binadamu.

Wanaharakati wa haki za binadamu na wataalam wa Umoja wa Mataifa wanakadiria kuwa angalau watu milioni moja kutoka jamii ya Uyghur wanashikiliwa katika kambi za Xinjiang, magharibi mwa China, ambapo inasemekana wanalazimishwa kufanya kazi nguvu, wanafanyiwa mateso na dhulma mbalimbali, madai ambayo China imefutilia mbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.