Pata taarifa kuu
CHINA-HAKI

China yamhukumu raia wa Canada Michel Spavor kwa ujasusi

Mahakama ya China imemkuta na hatia ya ujasusi mfanyabiashara wa Canada Michael Spavor leo Jumatano na kumhukumu kifungo cha miaka kumi na moja gerezani, na kuongeza kuwa itamfukuza nchini humo bila kutaja lini, kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti wa mahakama hiyo.

Maafisa wa usalama wanawasogeza waandishi wa habari mbali na gari ambalo linambeba Mcanada Michael Spavor katika korti ya Dandong Machi 19, 2021.
Maafisa wa usalama wanawasogeza waandishi wa habari mbali na gari ambalo linambeba Mcanada Michael Spavor katika korti ya Dandong Machi 19, 2021. © AP - Ken Moritsugu
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shrika la habari la REUTERS, wakili wa Beijing, Mo Shaoping, amesema kwamba hatua ya kumfukuza mhalifu inatekelezwa mara nyingi baada ya kumaliza kutumikia kifungo chake, lakini inaweza kutokea mapema katika baadhi ya kesi.

Hukumu hiyo inakuja wakati mawakili wa mkurugenzi wa kifedha wa kampuni kubwa ya simu ya China ya Huawei, Meng Wanzhou, wanajaribu kushawishi mahakama ya Canada kutompeleka nchini Marekani, ambayo inamshutumu kwa kukiuka vikwazo vya Marekani kuhusiana na Iran.

Mahakama ya Dandong imetangaza kuwa yuan 50,000 (euro 6,580) ya mali ya kibinafsi ya Michael Spavor itachukuliwa.

Michael Spavor na mwanadiplomasia wa zamani wa Canada Michael Kovrig walikamatwa nchini China siku chache baada ya kukamatwa kwa Meng Wanzhou nchini Canada.

Siku ya Jumanne, korti ya China iliidhinisha hukumu ya kifo ya raia wa Canada kwa biashara ya dawa za kulevya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.