Pata taarifa kuu
MAREKANI-KURDISTAN-IS-USALAMA

Mkuu wa Pentagon ziarani Kurdistan kuzungumzia IS

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Ashton Carter, Alhamisi hii, amekutana na rais wa Kurdistan nchini Iraq, Massoud Barzani, wakati wa ziara yake katika jimbo hilo linalojitegemea, kaskazini mwa Iraq. Mazungumzo ya viongozi hao yaligubikwa na vita dhidi ya kundi la Islamic State (IS).

Rais wa Kurdistan, Massoud Barzani (kulia) akimkaribisha kiongozi wa Pentagon, Ashton Carter, Desemba 17, 2015 katika Erbil.
Rais wa Kurdistan, Massoud Barzani (kulia) akimkaribisha kiongozi wa Pentagon, Ashton Carter, Desemba 17, 2015 katika Erbil. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Kikurdi nchini Iraq ni mshirika mkuu wa Washington, ambayo inaongoza muungano wa kimataifa dhidi ya IS nchini Iraq lakini pia nchini Syria.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa shirika la habari la Ufaransa la AFP, Bw Carter amekutana na Massoud Barzani, katika mji wa Erbil, mji mkuu wa Kurdistan, unaopatikana kwenye umbali wa zaidi ya kilomita mia moja kutoka Mosul, mji wa pili wa Iraq, ulioaanguka mikononi mwa kundi la Islamic State mwezi Juni 2014.

Jumatano wiki hii, IS ilikiri kuhusika na shambulizi dhidi ya kambi ya jeshi karibu na mji wa Mosul ambapo askari wa Uturuki wanapiga kambi, pamoja na operesheni nyingine dhidi ya kambi ya wapiganaji wa Kikurdi (Peshmerga) katika jimbo hilo.

Baraza la Usalama la Kurdistan (KRSC) hata hivyo limesema kwamba wapiganaji wa Kikurdi (Peshmerga) walikabiliana siku hiyo na mashambulizi kadhaa ya IS, nakufaulu kuyarejesha nyuma.

"Ilikuwa ni jaribio (la IS) kuvunja safu ya kujihami ya Peshmerga baada kupata hasara kubwa katika miezi ya hivi karibuni", Baraza hilo limesema.

Siku ya Jumatano, kiongozi wa Pentagon alifanya mazungumzo mjini Baghdad na Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, juu ya uwezo "wa kuboresha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja ya silaha na mafunzo", kwa mujibu wa ofisi ya Haider al-Abadi .

Rais wa Marekani Barack Obama alisema Jumatatu kuwa juhudi za kijeshi za Marekani na washirika wake dhidi ya IS ziliongezwa lakini alibaini kwamba maendeleo dhidi ya wanajihadi yanapaswa kufanyika "haraka".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.