Pata taarifa kuu
MAREKANI-IS-USALAMA

Obama: “mapambano dhidi ya IS yameongezeka”

Barack Obama amesema Jumatatu kuwa juhudi za kijeshi za Marekani na washirika wake dhidi ya kundi la Islamic State nchini Iraq na Syria zimeongezeka. Lakini ametambua kwamba maendeleo dhidi ya wanajihadi yanapaswa jufanyika kwa "haraka".

Rais wa Marekani Barack Obama mjini Washington Desemba 12, 2015.
Rais wa Marekani Barack Obama mjini Washington Desemba 12, 2015. AFP/AFP/
Matangazo ya kibiashara

"Tunawashambulia kwa nguvu zaidi", amesema rais wa Marekani akiwa Pentagon ambako amekutana na Baraza lake la Usalama wa kitaifa. "Kadri wanapokuwa dhaifu, itakuwa vigumu zaidi kwa (wapiganaji wa) IS kufanya propaganda zao duniani kote", Obama ameongeza.

Siku nane baada ya hotuba iliyotolewa katika Ofisi ya White House, Obama alitangaza kuwa Waziri wa Ulinzi Ashton Carter atajielekeza Jumatatu hii Mashariki ya Kati "kufanya kazi na washirika wa muungano ili kupata michango zaidi ya kijeshi ".

"Haya yanaendelea kuwa mapambano magumu", rais wa Marekani amekiri, na kubainisha kuwa wanajihadi wamekuwa wakitumia "wanaume, wanawake na watoto kama ngao zao."

Obama, ambaye anashindwa kuwashawishi Wamarekani kwa uhalali wa mkakati wake dhidi ya IS, amezungumza kwa kirefu juu ya mafanikio yaliyopatikana katika uwanja wa vita mwezi uliopita.

"IS imepoteza maeneo mengi kwa kilomita mraba ya maeneo iliyokua ikiyadhibiti nchini Syria(...). "Katika maeneo mengi, wamepoteza uhuru wao wa ujanja kwa sababu wanajua kwamba kama wataweka pamoja vikosi vyao, tutawaondoa" , Obama amesisitiza. "Tangu majira ya joto, IS imeshindwa kuendesha hata operesheni moja, iwe nchini Iraq au nchini Syria", ameongeza.

"Hata hivyo, tuna imani kutokana na maendeleo ambayo yanapaswa kufanywa kwa haraka", amemalizia Obama, huku akibainisha kuwa raia wa Iraq na Syria wanmekua wakiishi chini ya utawala wa "vitisho."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.