Pata taarifa kuu
IRAQ-IS-MAPIGANO-USALAMA

Vikosi vya Iraq vyaiteka sehemu kubwa ya Ramadi kutoka mikononi mwa IS

Vikosi vya Iraq vimeiteka sehemu kubwa ya mji wa Ramadi, iliyoko kilomita 100 magharibi mwa Baghdad, ambayo ilikua chini ya udhibiti wa wanajihadi tangu mwezi Mei, maafisa wa Iraq wamesema.

Roketi ikirushwa na vikosi vya Iraq karibu na mji wa Ramadi, Desemba 7, 2015.
Roketi ikirushwa na vikosi vya Iraq karibu na mji wa Ramadi, Desemba 7, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kuliteka eneo la Tamim ni mafanikio makubwa kwa vikosi vya Iraq ambavyo vilianzisha mashambulizi tangu miezi kadhaa iliyopita kwa lengo la kuurejesha chini ya himaya ya serikali halali mji wa Ramadi, mji mkuu wa jimbo la magharibi la Anbar.

"Leo hii, majeshi yetu yamelirejesha chini ya himaya yao eneo la Tamim baada ya mapigano makali dhidi ya wapiganaji Daech (ikimaanisha kwa neno fupi kwa Kiarabu IS)", msemaji wa kikosi maalum kinachopambana dhidi ya ugaidi cha Iraq, Sabah al-Nomane, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Kutekwa kwa eneo la Tamim pia kumethibitishwa na mkuu wa polisi wa mkoa wa Al Anbar, jenerali Hadi al-Irzayij pamoja na msemaji wa uongozi wa operesheni za kijeshi za pamoja.

Wapiganaji wa kundi la Islamic State wameyateka maeneo mengi nchini Iraq, ikiwa ni pamoja na mji wa pili wa nchi hiyo, Mosul, katika mashambulizi walioanzisha mwezi Juni mwaka 2014. Miezi sita kabla wapiganaji wa IS kuuteka mji wa Fallujah, uliyoko Anbar, mkoa mkubwa nchini.

Vikosi vya Kikurdi vinavyoungwa nkono na mashambilizi anga ya muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani viliuteka katikati mwa mwezi Novemba, mji wa Sinjar, kaskazini mwa Iraq.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.