Pata taarifa kuu
UTURUKI-IRAQ-USALAMA

Erdogan akataa kuondoa askari wa Uturuki kutoka kaskazini mwa Iraq

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefutilia mbali Alhamisi hii uwezekano wa kuondoa askari wake kutoka katika ardhi ya Iraq na kutangaza mkutano wa pande tatu utakaofanyika Desemba 21 kati ya viongozi wa Uturuki, Marekani na Wakurdi wa Iraq.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameapa kutowaondoa askari wake katika ardhi ya Iraq.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameapa kutowaondoa askari wake katika ardhi ya Iraq. REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

"Hakuna hoja yoyote kuwa Uturuki iondoe askari wake kutoka Iraq", rais wa Uturuki amesema katika mkutano na waandishi wa habari, akisisitiza kuwa askari hao walikuwa eneo hilo wala si kushiriki katika mapambano lakini kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa Kikurdi ambao wanapigana na wapiganaji wa kundi la Islamic State katika mkoa wanakoishi.

Jumatano wiki hii, rais Erdogan alisema kuwa askari wa Uturuki walitumwa tangu mwaka 2014 katika kambi ya jeshi ya Bachika, kaskazini mwa Iraq, kwa ombi la Serikali ya Iraq.

Jumamosi Wizara ya mambo ya nje ya Iraq ilimuitisha balozi wa Uturuki kwenda kuamuru kuondolewa kwa haraka mamia ya askari waliotumwa hasa karibu na mji wa Mosul, unaodhibitiwa na kundi la Islamic State.

Wizara ya mambo ya nje ya Iraq imethibitisha kuwa vikosi vya Uturuki viliingia nchini Iraq bila kuifahamisha serikali ya mjini Baghdad na kwamba Iraq imekua ikichukulia uwepo wa askari hawa kutoka Uturuki kama "kitendo cha uadui".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.