Pata taarifa kuu

Sudan: Msafara wa ICRC wakumbwa na shambulio mjini Khartoum

Nchini Sudan, msafara wa shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (ICRC) ulishambuliwa Jumapili Desemba 10, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua wawili na saba kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi watatu wa shirika la kibinadamu.

ICRC inafanya kazi nchini Sudan (picha ya kielelezo).
ICRC inafanya kazi nchini Sudan (picha ya kielelezo). AFP PHOTO/Waakhe WUDU
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hiyo ililenga kuwahamisha takriban watu mia moja waliokwama kwenye mapigano huko Khartoum, mji mkuu wa Sudan, kati ya jeshi la taifa na wanamgambo wa RSF. Lakini magari ya kibinadamu yalilengwa. ICRC imelaani vikali shambulio hilo.

ICRC inasema "imefadhaishwa na kushtushwa" na shambulio la msafara wake. Magari matatu na mabasi matatu yaalikuwa yanakwenda mjini Khartoum, katikawilaya ya Al-Shagara, kusafirisha karibu watu mia moja walio hatarini, hasa watoto, mayatima, wagonjwa na wazee, hadi eneo la Wad Madani, nje ya mji mkuu.

Lakini msafara huu wa magari sita, yote yakiwa na alama ya Msalaba Mwekundu, yalishambuliwa "yalipoingia katika eneo la ambako watu walitakiwa kuhamihwa", inaeleza ICRC. “Hili ni shambulio lisilokubalika. Nimeshtushwa na naumizwa na na tabia ya kutoheshimiwa kabisa nembo ya Msalaba Mwekundu ambayo lazima ilindwe kwa mujibu wa sheria za kibinadamu,” amejibu Pierre Dorbes, mkuu wa shirika hilo nchini Sudan. Operesheni hiyo ilibidi kusitishwa. ICRC inakumbusha, hata hivyo, kwamba uhamishaji huo ulikuwa umeombwa na kuratibiwa na wahusika kwenye mzozo ambao "walifikia makubaliano yao" na "kutoa dhamana ya usalama".

Jeshi lahusika kwa shambulio

Jeshi limekiri kuhusika na shambulio hilo. Vikosi vya Sudan vinasema msafara huo ulikiuka makubaliano kwa kukengeuka kutoka njia iliyopangwa, na kukaribia eneo la ulinzi na gari la waasi lililokuwa na bunduki. RSF, kwa upande wake, ilmebaini kwamba watu wao watano - walisindikiza msafara, kwa usalama, lakini hadi kikomo cha eneo lao. Kisha, ICRC iliendelea peke yake kama ilivyopangwa na jeshi likafyatua risasi kwenye magari yake, wamesema wanamgambo hao.

Matoleo mawili yanayopingana katika tukio ambalo linahatarisha mkutano unaotarajiwa kati ya viongozi wa kambi hizo mbili ndani ya siku 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.