Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa unahitaji dola bilioni 46.4 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu mwaka 2024

Jumatatu hii, Desemba 11, Umoja wa Mataifa ulizindua ombi la michango yenye thamani ya dola bilioni 46.4 kwa mwaka wa 2024,  ili kusaidia watu milioni 180.5 duniani. Bila ufadhili wa kutosha, "watu watakabiliwa na hali ngumu", umeonya Umoja wa Mataifa, ambao unaangazia kuongezeka kwa migogoro, dharura ya tabi nchi au hata kuporomoka kwa uchumi, linaripoti shirika la habari la AFP.

Martin Griffiths pia ameangazia mahitaji ya Burma, Ukraine ambayo inapitia "majira ya baridi kali" yenye matarajio ya kuimarika kwa vita, na Sudan ambayo amesema haipati msaada unaostahili kutoka katika nchi za Magharibi.
Martin Griffiths pia ameangazia mahitaji ya Burma, Ukraine ambayo inapitia "majira ya baridi kali" yenye matarajio ya kuimarika kwa vita, na Sudan ambayo amesema haipati msaada unaostahili kutoka katika nchi za Magharibi. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Iwapo macho yote kwa sasa yanaelekezwa katika vita vya Ukanda wa Gaza, Umoja wa Mataifa unakumbusha kuwa Mashariki ya Kati, Sudan na Afghanistan pia zimenufaika na oparesheni muhimu za misaada ya kimataifa. Hata hivyo, ukubwa wa wito wa kila mwaka na idadi ya walengwa ambao Umoja wa Mataifa unataka kusaidia imepunguzwa ikilinganishwa na mwaka 2023, kutokana na michango michache.

"Wasaidizi wa kibinadamu wanaokoa maisha ya watu, wanapambana na njaa, wanalinda watoto, wanakabiliana na milipuko ya magonjwa, na kutoa makazi na usafi wa mazingira katika hali zisizo za kibinadamu," mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu Martin Griffiths, amesema katika taarifa yake. "Lakini msaada unaohitajika kutoka kwa jumuiya ya kimataifa haukidhi mahitaji," amelaumu.

Umoja wa Mataifa ulikuwa umetoa wio wa dola bilioni 56.7 kwa mwaka wa 2023, lakini ulipata 35% tu, upungufu mbaya zaidi wa ufadhili tangu miaka kadhaa iliyopita. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yalitoa msaada na ulinzi kwa watu milioni 128. Na mwaka 2023 uko mbioni kuwa mwaka wa kwanza tangu mwaka 2010 ambapo michango ya misaada ya kibinadamu imepungua ikilinganishwa na mwaka uliopita. Pia, kwa mwaka 2024, Umoja wa Mataifa umeamua kupunguza wito wake wa michango, ikichagua kuzingatia mahitaji ya haraka zaidi.

Nchi 72 zahitaji msaada

Wito wa michango unalenga kufadhili shughuli katika nchi 72: nchi 26 zilizo katika mgogoro na nchi 46 jirani ambazo zinakabiliwa na athari, kama vile wimbi la wakimbizi. Nchi inayoongiza ni Syria (dola bilioni 4.4), ikifuatiwa na Ukraine (bilioni 3.1), Afghanistan (bilioni 3), Ethiopia (bilioni 2.9), na Yemen (bilioni 2.8).

Kunaweza kuwa na karibu watu milioni 300 wanaohitaji msaada ulimwenguni kote mnamo 2024, kulingana na Martin Griffiths. Lakini Umoja wa Mataifa utaelekeza nguvu zake tu kwa milioni watu 180.5 kati yao, wengine pia wanaweza kupata usaidizi kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika mengine pamoja na nchi zenyewe.

Waathirika wa hali ya hewa

Eneo la kwanza la kijiografia linalohusika na wito huu wa fedha ni Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini (bilioni 13.9). Lakini Martin Griffiths pia ameangazia mahitaji ya Burma, Ukraine ambayo inapitia "majira ya baridi kali" yenye matarajio ya kuimarika kwa vita, na Sudan ambayo amesema haipati msaada unaostahili kutoka katika nchi za Magharibi.

Kuhusu Venezuela, afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema anatumai kuwa mazungumzo ya kisiasa yatafungua kupatikana kwa mali zilizozuiwa na kuwa "mfano mzuri wa mazungumzo ya kuleta matunda mazuri kwa kijamii".

Nchini Afghanistan, amesema kwamba ikiwa uwekezaji wa kiuchumi unaweza kufanywa bila kupoteza mwelekeo wa haki za binadamu, jumuiya ya kimataifa inaweza kuepuka njaa inayoweza kutokea kwa gharama ya chini.

Mahitaji yanayohusiana na athari za mabadiliko ya tabia nchi pia yanazidi kuwa muhimu. "Hakuna shaka kuwa hali ya hewa inashindana na migogoro kama kichocheo cha mahitaji," amebainisha. "Hali ya hewa inawahamisha watoto zaidi sasa kuliko migogoro. Haijawahi kuwa hivi huko nyuma.”

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.