Pata taarifa kuu

Djibouti: IGAD kujadili mzozo wa Sudan

Mkutano wa kilele usio wa kawaida wa wakuu wa nchi na serikali wa Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD) umefunguliwa Jumamosi hii, Desemba 9 nchini Djibouti. Taasisi ya kikanda ya Pembe ya Afrika inachunguza mzozo wa Sudan, siku chache baada ya kushindwa kwa mazungumzo huko Jeddah, nchini Saudi Arabia.

Moshi mwingi unaosababishwa na mapigano unaelea juu ya Khartoum (picha ya Juni 2023). Mkutano wa kilele usio wa kawaida wa IGAD unafunguliwa Desemba 9 nchini Djibouti kuhusu hali ya Sudan.
Moshi mwingi unaosababishwa na mapigano unaelea juu ya Khartoum (picha ya Juni 2023). Mkutano wa kilele usio wa kawaida wa IGAD unafunguliwa Desemba 9 nchini Djibouti kuhusu hali ya Sudan. © File photo/AP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Gaëlle Laleix

Mkutano huu wa kilele wa IGAD utatoa mwelekeo mpya wa upatanishi wa kikanda katika mgogoro wa Sudankulingana na vyanzo vilivyo karibu na taasisi hiyo ya kikanda. Haya yanajiri baada ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, mkuu wa jeshi la Sudan kukutana kwa mazungumzo na wakuu wa nchi za ukanda huo. Alisafiri hadi Kenya mwishoni mwa mwezi wa Novemba kukutana na Rais William Ruto.

Kukataa upatanishi

Mkuu wa jeshi la Sudan, hata hivyo, alikataa upatanishi wa IGAD inayoongozwa na rais wa Kenya, ambaye aliituhumu kumuunga mkono mpinzani wake, Mohammed Hamdan Daglo, mkuu wa Rapid Support Forces (FSR). Kwa hivyo ni nini kilibadilisha msimamo wa Jenerali al-Burhan? "Kushindwa"… kinajibu chanzo cha kidiplomasia kutoka eneo hilo. "Baada ya kupoteza Khartoum na Darfur, Abdel Fattah al-Burhan labda anataka kuanzisha mijadala, kuwa na muda wa kununua silaha," kimesema chanzo hiki.

Jitihada zisizoeleweka wakati mazungumzo ya Jeddah chini ya uangalizi wa Marekani na Saudi Arabia yameshindwa. "Nchi za Ghuba ni sehemu ya tatizo," kinaendelea chanzo hiki, "haziwezi kutatua tatizo ikiwa ikiwa wao ndio chanzo cha tatizo hilo. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.