Pata taarifa kuu

Somalia: Askari kadhaa wa kikosi cha makomando wakamatwa kwa kuiba mgao wa chakula

Askari wa kikosi cha makomando wa Kisomali waliofunzwa na Marekani wamekamatwa kwa kuiba chakula, maafisa wawili wa Somalia wamesema siku ya Ijumaa.

Wanachama wa vikosi vya usalama vya Somalia, hapa wakishika doria mjini Mogadishu, Februari 21, 2023.
Wanachama wa vikosi vya usalama vya Somalia, hapa wakishika doria mjini Mogadishu, Februari 21, 2023. AP - Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Marekani imekuwa muungaji mkono mkuu wa makomando wa Kisomali wa Brigedi ya Danab, jeshi la wasomi waliohusika katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali Al Shabab. Siku ya Alhamisi Wizara ya ulinzi ya Somalia ilisema kwamba jeshi "limeripoti matumizi mabaya ya mgao ndani ya kitengo cha vikosi vya Danab," na kusababisha serikali kuanzisha uchunguzi ambao ulisababisha kusimamishwa kazi na kukamatwa kwa maafisa kadhaa.

"Serikali ya shirikisho, kwa makubaliano na serikali ya Marekani, itachukua jukumu la kutoa mgao wa chakula kwa Danab," imesema. Washington ilianza kusaidia kikosi cha Danab mnamo 2017, kutoa mafunzo kwa kitengo cha wasomi na kukipatia vifaa vya kijeshi na chakula.

Makomando hawa walikuwa na jukumu muhimu katika mashambulizi ya hivi karibuni ya kijeshi ya Somalia dhidi ya Al Shabab. Kwa mujibu wa maafisa wa Somalia waliozungumza na shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa majina, wizi huo katika duka la kijeshi mjini Mogadishu uligunduliwa mwezi Desemba 2023.

"Serikali ya Marekani ilidai uchunguzi wa kina na serikali ya Somalia iliongoza uchunguzi ili kuepuka kusimamishwa kwa msaada wa serikali ya Marekani kwa jeshi la Somalia," afisa mkuu wa jeshi la Somalia ameliambia shirikala habari la AFP.

Afisa katika Wizara ya Ulinzi ameeleza kuwa "Marekani iliifahamisha serikali ya Somalia kwamba itasitisha msaada wake kwa kikosi cha Danab ikiwa serikali ya Somalia itashindwa kubaini ukweli na kupata waliohusika."

"Lakini sasa swali hili limetatuliwa: wale waliohusika wamekamatwa na watafikishwa mahakamani," imeliambia shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.