Pata taarifa kuu

Sudan: Al-Burhan na "Hemedti" wakubaliana kukutana mwishoni mwa mkutano wa kilele wa IGAD

Majenerali wanaopigania madaraka nchini Sudan Abdel Fattah al-Buran na Mohamed Hamdan Daglo, anayejulikana kama "Hemedti", wamekubali kukutana,  klingana na taarifa kwa kutoka Jumuiya ya maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki (IGAD) siku ya Jumapili Desemba 10, 2023 kufuatia mkutano wa kilele usio wa kawaida uliofanyika nchini Djibouti.

Majenerali wanaopigania madaraka nchini Sudan Abdel Fattah al-Burhan (kushoto) na Mohamed Hamdan Daglo anayejulikana kama "Hemedti" (kulia).
Majenerali wanaopigania madaraka nchini Sudan Abdel Fattah al-Burhan (kushoto) na Mohamed Hamdan Daglo anayejulikana kama "Hemedti" (kulia). © AP Photo - Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Gaëlle Laleix

Haya ni mafanikio ya kidiplomasia ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwa IGAD kumaliza vita nchini Sudan, ambavyo vimedumu kwa miezi saba. Hadi sasa, majadiliano yote yameshindwa, ikiwa ni pamoja na yale ya Jeddah, chini ya  mwamvuli wa Washington na Riyadh.

Wawili hao walikubaliana kukutana ndani ya wiki mbili, mkutano ambao ulionekana kutofikirika chini ya wiki moja kabla, wakati majadiliano ya Jeddah yalipokoma. Kwa hivyo IGAD imepata mafanikio makubwa ya kidiplomasia.

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mzozo huo, Abdel Fattah al-Burhan alikuwepo wakati wa mkutano huu usio wa kawaida wa IGAD. Kuhusu Mohamed Hamdan Daglo, anayejulikana kama "Hemedti", alizungumza kwa simu na wakuu wa serikali wa jumuiya hiyo, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari.

Kwenye ukurasa wake wa X (zamani ikiitwa Twitter) Baraza la mpito limetbibitisha kujitolea kwa Jenerali Abdel Fattah al-Burhan kutia saini kwenye makubaliano ya usitishwaji wa mapigano, pendekezo ambalo Jenerali Mohamed Hamdan Daglo amekubali katika barua aliyorusha kwenye mtandao huo wa kijamii.

Lakini sasa tunapaswa kushughulika na manukuu ya kila mtu. Kulingana na Gazeti la Sudan Tribune, mkuu wa jeshi la Sudan, kwa mfano, anaomba kwamba wapiganaji wa RSF wajitoe kwenye maeneo walikotakwa kukusanywa. Katika barua yake, Mohamed Hamdan Daglo anatoa wito wa kukamatwa kwa viongozi wa zamani wa utawala uliopita.

Takriban wanadiplomasia kumi na watano wa Imarati walitangazwa kuwa ni watu wasiotakiwa nchini Sudan na serikali ya nchi hiyo, ambayo inashutumu Abu Dhabi kwa kuipatia RSF silaha.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ilitangaza takriban wanadiplomasia kumi na watano kutoka Falme za Kiarabu watu wasiotakiwa nchini Sudan, kulingana na tangazo la Jumapili Desemba 10 kutoka kwa shirika la habari la serikali la SUNA.

Nchi hizo mbili zilipazaa sauti tangu afisa mkuu wa jeshi aliposhutumu Abu Dhabi wiki iliyopita kwa kusambaza silaha kwa RSF. Maandamano yalifanyika katika mitaa ya Port Sudan, ambayo imekuwa mji mkuu wa utawala wa nchi hiyo tangu mzozo huo, kumtaka balozi wa Imarati aondoke. Wanadiplomasia 15 waliofukuzwa sasa wana saa 48 kuondoka Sudan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.