Pata taarifa kuu
USALAMA-UGAIDI

Wapiganaji watano wa kundi la Boko Haram wauawa kusini mashariki mwa Niger

Wapiganaji watano wa kundi la wanajihadi la Boko Haram waliuawa na wanajeshi wawili wa Niger kujeruhiwa katika mapigano ya yaliyotokea siku ya Alhamisi kusini mashariki mwa Niger, karibu na Nigeria, shirika la habari la AFP likinukuu mamlaka za ndani siku ya Ijumaa.

Mwanajeshi wa Niger akitoa ulinzi kwenye barabara karibu na soko huko Banibangou, mji ulioko magharibi mwa Niger, mnamo Novemba 6, 2021, ambapo watu 69 waliuawa katika shambulio la wanajihadi mnamo Novemba 2, 2021.
Mwanajeshi wa Niger akitoa ulinzi kwenye barabara karibu na soko huko Banibangou, mji ulioko magharibi mwa Niger, mnamo Novemba 6, 2021, ambapo watu 69 waliuawa katika shambulio la wanajihadi mnamo Novemba 2, 2021. AFP - BOUREIMA HAMA
Matangazo ya kibiashara

"Ngome ya Walinzi wa Kitaifa ilikabiliwa na mapigano mawili kati ya (maeneo) ya Bagué na Tchoungoua. Tuna majeraha madogo mawili kwenye upande wa wanajeshi na kwa upande wa adui, wapiganaji watano wa Boko Haram waliuawa", alibainisha Smain Younous, aliyeteuliwa kuwa gavana mpya wa mkoa wa Diffa, katika mwa mwezi wa Novemba.

Bunduki nne aina ya AK47 zilinaswa na wanajeshi wa Niger. Diffa, jiji kubwa lililoko kusini-mashariki mwa Niger, ni mwenyeji wa michuano ya kila mwaka ya mieleka ya kitamaduni, mchezo muhimu nchini humo, ambao watashiriki wanamieleka themanini kutoka mikoa minane ya Niger. Michuano hii inaanza siku ya Ijumaa Desemba 23, 2022.

"Vikosi vya ulinzi na usalama vinadhibiti kila pembe" ya eneo la Diffa, amehakikisha Gavana Smain Younous. Mapigano ya Alhamisi yanakuja baada ya wiki za utulivu katika eneo la Diffa, ambalo pia mwaka huu limekumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababishwa na kuja kwa mto Komadougou Yobé.

Mwishoni mwa Septemba, wakulima kumi na moja, Waniger tisa na Wanigeria wawili, "waliuawa kwa risasi" na washukiwa wa wanajihadi karibu na Toummour, mji ulioko katika jimbo la Diffa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.