Pata taarifa kuu

Watu saba wafariki katika mlipuko wa lori la mafuta nchini Niger

Watu saba wamefariki dunia wakati lori la mafuta lilipolipuka karibu na kijiji kimoja katika mkoa wa Zinder kusini-kati mwa Niger, limebaini shirika la habari la AFP likinukuu viongozi kutoka eneo hilosiku ya Jumatatu.

Nchini Niger, lori lamafuta lililokuwa likisheheni lita 36,000 za petroli lilipinduka mbele ya kituo cha mafuta huko Niamey mnamo Mei 6, 2019.
Nchini Niger, lori lamafuta lililokuwa likisheheni lita 36,000 za petroli lilipinduka mbele ya kituo cha mafuta huko Niamey mnamo Mei 6, 2019. RFI/Moussa Kaka
Matangazo ya kibiashara

"Watu saba walifariki dunia katika mlipuko wa lori la mafuta lililoharibika walipokuwa wakichota mafuta," afisa mmoja katika mkoa wa Zinder amesema. Watu watano walifariki papo hapo na wengine wawili kufariki dunia katika kituo cha afya kutokana na majeraha ya kuungua walioyapata, ameongeza.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi wakati injini ya pikipiki iliyokuwa ikikimbia kwa kasi iliwaka na kusababisha lori hilo kuwaka moto na kulipuka. Wanakijiji walikuwa wakichota mafuta yaliyokuwa yakivuja wakati wa mlipuko huo, kwa mujibu wa televisheni ya serikali ya Niger ambayo ilmerusha hewani picha za lori hilo lililopinduka barabarani. Ilikuwa imebeba lita 64,000 za petroli na ilikuwa ikisafiri kuelekea Niamey ilipopinduka.

Zinder ndipo kunapatikan kampuni ya Kusafisha mafuta ya Zinder (Soraz), kilomita 1,000 kutoka mji mkuu wa Niger. Matukio yanayohusishwa na mlipuko wa lori zilizobeba mafuta hutokea mara kwa mara nchini Niger, mzalishaji mdogo wa dhahabu nyeusi tangu 2011.

Mnamo Mei 2019, watu 76 walifariki dunia na karibu 40 waliungua vibaya huko Niamey wakati lori la mafuta lililokuwa likisafirisha lita 50,000 za petroli kwenda nchi jirani ya Burkina Faso lilipopuka. Kabla ya mlipuko huo, watu walikataa kutii maagizo ya polisi ambayo ilitaka kuwaepusha na hatari ya moto.

Dereva wa pikipiki ambaye alikuwa ametoka kujaza madumu mafuta alisababisha mlipuko huo alipokuwa akijaribu kuwasha pikipiki yake kulingana na shuhuda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.