Pata taarifa kuu

Niger yapokea helikopta mbili kutoa Ufaransa kwa ajili ya mapambano dhidi ya wanajihadi

Niger imepokea helikopta mbili za kivita za Gazelle na vipuri vyake, vilivyotolewa na Ufaransa kwa msaada wa jeshi lake dhidi ya makundi ya wanajihadi, hasa magharibi karibu na Mali, shirika la habari la AFP limenukuu Alhamisi hii Wizara ya Ulinzi ya Niger.

Helikopta mbili za kivita za Gazelle za jeshi la Ufaransa nchini Niger.
Helikopta mbili za kivita za Gazelle za jeshi la Ufaransa nchini Niger. RFI/Olivier four
Matangazo ya kibiashara

Msaada huu unafikisha tano idadi ya helikopta za Gazelle zilizotolewa na Paris kama sehemu ya mradi wa "Mafunzo ya Helikopta" kwa jeshi la Niger ambapo Ufaransa tayari imewekeza euro milioni 24, alisema Sylvain Itté, balozi wa Ufaransa katika hafla ya kukabidhi helikopta hizo mbili siku ya Jumatano.

Waziri wa Ulinzi wa Niger, Alkassoum Indatou, alipongeza "msaada huu mpya" wa helikopta ambao "unajumuisha uthibitisho wa msaada usio na masharti" wa Ufaransa "katika mapambano dhidi ya ugaidi".

Waziri huyo pia alikaribisha "ushirikiano kati ya majeshi ya Niger na Ufaransa", ambayo yamewezesha wakulima katika eneo la Tillabéri (magharibi), karibu na mpaka wa Mali kulima mashamba yao "kwa utulivu kamili" mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.