Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Jeshi la Niger ladai kuwaua wanajihadi 15 karibu na Mali

Jeshi la Niger limesema siku ya Ijumaa kuwa limewaua washukiwa kumi na watano wa kijihadi wakati wa "mashambulizi" yaliyofanywa kwa ushirikiano na wanajeshi wa Ufaransa karibu na Mali, katika eneo la "mipaka mitatu", mwishoni mwa wiki iliyopita.

Wanajeshi wa Niger huko TillabΓ©ry.
Wanajeshi wa Niger huko TillabΓ©ry. Β© RFI
Matangazo ya kibiashara

"Ujumbe wa Operesheni Almahaou (operesheni ya kupambana na wajihadi nchini Niger) ulishambuliwa katika eneo la Zibane na magaidi waliokuwa kwenye pikipiki. Mashambulizi ya angani na washirika yalifanya iwezekane kuwaangamiza magaidi kumi na watano", taarifa ya makao makuu ya jeshi iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP inabaini.

Aidha, pikipiki kumi na tano ziliharibiwa, bunduki kumi na mbili za Kalashnikov zilipatikana na vifaa mbalimbali vya mawasiliano na kinga vilikamatwa wakati wa operesheni hii, imesema taarifa hiyo.

Kulingana na afisa wa Niger, wanajeshi kutoka Operesheni ya vikosi vya Ufaransa- Barkhane - ambayo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza siku ya Jumatano kumalizika- walishiriki katika mashambulizi haya karibu na eneo la Anzourou, katika mkoa wa TillabΓ©ri, mji mkubwa magharibi mwa Niger , kama kilomita mia moja kutoka mpaka wa Mali.

Vijiji kadhaa karibu na Anzourou vimekumbwa na mashambulizi kadhaa. Mnamo Mei 2020, watu 20 waliuawa kwa kuchinjwa na watu wenye silaha waliiokuwa kwenye pikipiki, huko Zibane na vijiji vingine viwili jirani. Mnamo Agosti 2021, watu 19 waliuawa na wengine wawili kujeruhiwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi "waliokuja kwa miguu" katika kijiji cha Theim, katika mji huo.

Takriban wanajeshi 3,000 wa Ufaransa wametumwa katika ukanda wa Sahel - ikiwa ni pamoja na 1,730 nchini Niger, mmoja wa washirika wakuu wa Paris - baada ya kuondoka kabisa nchini Mali.

Kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba, "operesheni za pamoja" kumi na tano zilifanywa na wanajeshi wa Niger na Ufaransa magharibi mwa Niger, kwenye mpaka na Mali, eneo ambalo kwa miaka mingi limekuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa makundi ya wanajihadi, makao makuu ya jeshi yalitangaza mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.