Pata taarifa kuu
MAREKANI-ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Marekani kufungua rasmi ubalozi wake Jerusalem

Marekani inatarajia kufungua rasmi siku ya Jumatatu wiki ijayo ubalozi wake Jerusalem, licha ya hatua hiyo kupingwa na jumuiya ya kimataifa na Palestina, hali ambayo huenda ikasababisha kuzuka kwa mvutano mkubwa wa kikanda.

Mnamo Mei 7, 2018, wafanyakazi waliweka mabangoya kwanza yanayoonyesha eneo kunakopatikana ubalozi wa Marekani ambao utafunguliwa Mei 14 kufuatia uamuzi uliokaribishwa kama wa kihistoria na Israeli na kushtumiwa na jumuiya ya kimataifa.
Mnamo Mei 7, 2018, wafanyakazi waliweka mabangoya kwanza yanayoonyesha eneo kunakopatikana ubalozi wa Marekani ambao utafunguliwa Mei 14 kufuatia uamuzi uliokaribishwa kama wa kihistoria na Israeli na kushtumiwa na jumuiya ya kimataifa. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya Marekani ya kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem ni katika kutekeleza ahadi ya Rais Donald Trump Desemba 6 ya kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli.

Hatua hii ya Marekani imeridhisha Israel lakini Palestina na baadhi ya nchi za Kiarabu wameendelea kunung'unika.

Ufunguzii huu utaendana na kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 70, kulingana na kalenda ya Gregory, ya kuundwa kwa taifa la Israeli. Siku ya kufuatia, Wapalestina wataadhimisha "Nakba" ("Mateso" katika ulimwengu wa Kiarabu), kuondoka kwa mamia ya maelfu yao baada ya kufukuzwa au kuyahama makazi yao mnamo mwaka 1948.

Ufunguzi huo utafanyika katika wakati ambapo mvutano kati ya Israeli na Palestina unaendelea. Wapalestina wamekuwa wakiandamana kwa wiki kadhaa katika Ukanda wa Gazawakitaka iheshimiwe mipaka ya mwaka 1948.

Wapalestina zaidi ya 50 wameuawa na jeshi la Israeli wakati wa maandamano yaliyoanza tangu Machi 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.