Pata taarifa kuu
UGANDA-HAKI-USALAMA

Ukandamizaji dhidi ya watu wa mapenzi wa jinsia moja waendelea Uganda

Uganda imeendelea kukosolewa kuhusu hatua yake ya kuwakamata na kuendelea kuwazuia watu sitini na saba kwa madai kuwa wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Jiji la Kampala, mji mkuu wa Uganda (picha ya kumbukumbu).
Jiji la Kampala, mji mkuu wa Uganda (picha ya kumbukumbu). © REUTERS/James Akena/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Hivi kaibuni jaribio la Waziri wa maadili wa Uganda Simon Lokodo kupitisha tena sheria ya mwaka 2014 ya kuruhusu adhabu ya kifo kwa watu waliokutwa na hatia ya kufanya mapenzi ya jinsia moja ilichochea shutuma kali katika taifa hilo la Afrika mashariki kutoka kwa jamii ya walio wachache

Jumapili Novemba 10 polisi ya Uganda iliwakamata watu 67 katika baa moja jijini Kampala, sehemu maarufu kwa jamii ya jamii ya watu wa mapenzi wa jinsia moja (LGBT).

Shirika moja la haki za binadamu nchini Uganda, limesema hakuna shaka kuwa kuwafungulia mashitaka watu hawa 67, viongozi wametaka kuwafanya vitisho jamii ya watu wa mapenzi wa jinsia moja (LGBT).

Wanaume 61 na wanawake 6 walikamatwa Jumapili katika baa Ram Bar jijini Kampala. Watu wengine 58 walikamatwa wakati huo huo kabla ya kuachiliwa haraka.

Mwezi uliopita, watu 16 kutoka jamii hiyo ya walio wachache (LGBT) walilazimishwa kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu kwenye sehemu zao za siri (mbele na nyuma) baada ya kukamatwa. Kulingana na shirika la linalotetea jamii hiyo ya mashoga (Sexual Minorities Uganda), mashambulizi dhidi ya watu wa mapenzi wa jinsia moja yameongezeka katika wiki za hivi karibuni, haswa tangu Waziri wa Maadili wa Uganda kutangaza mpango wa kuanzisha tena sheria inayopinga mahusiano ya jinsia moja iliyofutwa na Mahakama ya Katiba mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.