Pata taarifa kuu
KENYA-UHURU KENYATTA-DENI

Rais Kenyatta kuiachia Kenya deni la Dola Bilioni 70 atakapoondoka madarakani 2022

Ripoti ya Wizara ya fedha nchini Kenya, inaonesha kuwa, rais Uhuru Kenyatta, ataacha deni la Dola Bilioni 70 wakati atakapoondoka madarakani mwezi Agosti mwaka 2022 baada ya muhula wake wa pili kukamilika.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati akiwasili katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi 2017
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati akiwasili katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi 2017 REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Deni hili linamaanisha kuwa walipa kodi nchini humo wataendelea kutoa fedha zaidi ili kulipa deni hilo. Hili litafanyika kupitia ongezeko la utozwaji kodi.

Serikali ya Kenya imekuwa ikisema imekuwa ikikopa fedha tangu mwaka 2013 ili kutekeleza ajenda yake hasa ujenzi wa miundo mbinu kwa kujenga barabara mpya, reli ya kisasa na kuhakikisha kuwa wananchi wengi wanaunganishwa na nguvu ya umeme.

Baada ya kuingilia madarakani mwaka 2013, rais Kenyatta alikopa Dola za Marekani Bilioni 3.6 kutoka kwa serikali ya China na kujenga reli ya kisasa kutoka Mombasa kwenda jijini Nairobi.

Kwa sasa, kiasi kikubwa cha fedha kinachopatikana kutokana na utozwaji wa kodi kwa wananchi, zinatumiwa kulipa madeni huku kinachosalia kikitumiwa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Rais Kenyatta, amekuwa akijitetea akisema ili kutekeleza ajenda nne za serikali yake, afya, chakula, uzalishaji na makaazi nafuu ni sharti Wakenya wahusike pakubwa kwa kulipa kodi zaidi.

Bunge hivi karibuni ilipitisha mswada wa fedha unaongeza kodi katika bidhaa za mafuta, ada ya kutuma na kupokea fedha kupitia simu za mkononi na ununuzi wa vifurushi vya Internet.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.