Pata taarifa kuu
TANZANIA-UFARANSA

Balozi Berak: Ufaransa itaimarisha uhusiano wa kibiashara na Tanzania ni muhimu

Nchi ya Ufaransa inasema kuwa, licha ya kwamba biashara inayofanya na Tanzania haiko kwenye kiwango cha kuridhisha, bado nchi hiyo inaona kuna uwezekano mkubwa wa uhusiano wa kibiashara uliopo kuboreka zaidi na kuzinufaisha nchi hizo

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Malika Berak. Machi 30, 2017
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Malika Berak. Machi 30, 2017 Emmanuel Makundi/RFIKiswahili
Matangazo ya kibiashara

Haya yamesemwa wakati huu nchi ya Ufaransa, Juma lijalo inaanza kuadhimisha wiki ya Ufaransa “Semain de la France” ambapo imeandaa mkutano wa kwanza wa kibiashara kati yake na Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Malika Berak, amesema mkutano wa juma lijalo utawakutanisha wafanyabiashara zaidi ya 200 na makampni zaidi ya 50 ya Ufaransa, ambapo kwa pamoja watajadili fursa za maendeleo zilizopo nchini Tanzania na kushirikiana.

Baliz Berak amesema uwepo wa makampuni hayo kunatoa fursa nzuri ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ufaransa kwenye biashara na uwekezaji.

"Kuna mchanganyiko unaowezekana na ni wazi hatuwezi kusahau kuwa Tanzania hadi hivi sasa..na sio kuwa itabakia hivi siku zote..ni nchi masikini lakini yenye rasilimali zinazoweza kuleta mageuzi makubwa kwenye nchi hii," alisema balozi Berak.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha biashara kwenye ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania Beatrice Alperte, amesema kwa sasa biashara inayofanyika kati ya nchi hizo mbili hairidhishi lakini wanaona kupitia kongamano hili mambo huenda yakabadilika.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Malika Berak (katikati), Beatrice Alpert, (kushoto wa kwanza) mkuu wa kitengo cha biashara. Machi 30, 2017
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Malika Berak (katikati), Beatrice Alpert, (kushoto wa kwanza) mkuu wa kitengo cha biashara. Machi 30, 2017 Emmanuel Makundi/RFIKiswahili

"Leo hii uhusiano wa kibiashara kati yetu na Tanzania uko chini sana na sio wa kuridhisha. Biashara tunayofanya inafikia Euro milioni 200, na zaidi tunatoa madawa na tunaagiza mazao ya kilimo japo sio kwa kiwango kikubwa. Tunadhani sasa ambapo Tanzania iko tayari kuingia kwenye mageuzi ya viwanda ni njia kwetu sisi kusonga mbele na tuwe na mazungumzo yaliyo kwenye mfumo mzuri," alisema Alperte.

Wataalamu wa masuala ya uchumi wanasema kuwa mkutano huu uwe ni fursa kwa nchi ya Tanzania kuieleza dunia kuhusu maboresho ambayo yamefanyika mpaka sasa kuvutia wawekezaji na makampuni kutoka nje.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.