Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI

Waasi wafanikiwa kuvirudisha nyuma Vikosi vya Syria huko Baba Amr wakati huu Misaada ikitarajiwa kuwafikia waathirika

Majeshi ya Tiifu kwa Rais wa Syria Bashar Al Assad yamerudishwa nyuma kwenye Wilaya ya Baba Amr iliyopo katika Jiji la Homs baada ya Waasi kujipanga upya na kufanikiwa kurejesha tena eneo hilo kwenye himaya yao wakati huu misaada ya kibinadamu ikitarajiwa kuwafikia waathirika wa machafuko hayo. Baraza la Taifa la Waasi Nchini Syria SNC limethibitisha wapiganaji wake kufanikiwa kuichukua tena Wilaya ya Baba Amr baada ya hiyo jana kuchukuliwa na Jeshi la Syria lakini pia wameonya kutakuwa na umwagaji mkubwa wa damu iwapo mapambano hayo yanateendelea.

Mashambulizi ambayo yanaendelea katika Wilaya ya Baba Amr yamezidi kuleta madhara wakati huu misaada ikitarajiwa kusambazwa
Mashambulizi ambayo yanaendelea katika Wilaya ya Baba Amr yamezidi kuleta madhara wakati huu misaada ikitarajiwa kusambazwa REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hizi zimetolewa wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN likitaka mapigano yasimame na hivyo kuruhusu misaada kuwafikia waathirika wanaohitaji huduma za haraka za kibinadamu hasa katika Jiji la Homs linaloshuhudia mashambulizi ya mabomu.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN kwenye taarifa yake limethibitisha China na Urusi kuunga mkono azimio hilo la kusitishwa kwa mapigano ili misaada iweze kuwafikia wananchi wanaotaabika kutokana na machafuko yanayoendelea huko Syria.

Balozi wa Uingereza kwenye Umoja wa Mataifa UN Mark Lyall Grant ambaye alikuwa Rais wa Kikao hicho amesema wao wanaendelea kusitikishwa kutokana na serikali ya Syria kuendelea kuwa kikwazo cha misaada kuweza kuwafikia wananchi walioathiriwa.

Licha ya kusikitishwa na kile kinachoendelea lakini Baraza la Usalama kwa kauli moja limelaani kitendo cha serikali ya Syria kukataa kumpa kibali cha kuingia nchini humo Mkuu wa Tume ya Misaada wa Umoja huo Valerie Amos.

Marekani kupitia Msemaji wake wa Wizara ya Mambo ya Nje Victoria Nuland imesema imeridhishwa na hatua ya serikali ya Syria kuwa tayari kuruhusu misaada kuweza kuwafikia wananchi huko Baba Amr.

Naye Msemaji wa Shirika la Mwezi Mwekundu pamoja na Msalaba Mwekundu Saleh Dabbakeh amesema wanaingia kwenye Wilaya ya Baba Amr hii leo kuweza kutoa misaada kwa wananchi waliojeruhiwa na hata wale wanaohitaji misaada.

Katika hatua nyingine Mpatanishi wa Umoja wa Mataifa UN kuhusu Mgogoro wa Syria ambaye ni Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja huo Kofi Annan ameendelea kusisitiza pande zinazokinzana kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kupata suluhu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.