rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani China Jim Mattis Xi Jinping

Imechapishwa • Imehaririwa

Mkuu wa Pentagon azuru China

media
Mkuu wa Pentagon azuru Beijing, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2014. © AFP

Waziri wa Ulinzi wa China, Wei Fenghe, amempokea Jumatano wiki hii mjini Beijing mwenzake wa Marekani, Jim Mattis na amesema ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ni muhimu sana.


Waziri wa Ulinzi wa China amezitaka nchi hizi mbili kuheshimiana, huku akibaini kwamba China iko tayari kutetea uhuru wake na usalama.

Kiongozi wa Pentagon pia amekutana na rais Xi Jinping, ambaye amesema "uhusiano wa China na Marekani ni miongoni mwa mambo muhimu zaidi duniani".

Kiongozi wa China amehakikisha kuwa nchi yake inatarajia kufanya kazi kwa utulivu wa kimataifa na amani. "Lakini hatuwezi kuacha inchi moja ya ardhi iliyoachwa na babu zetu," kiongozi wa China amesema, akimaanisha kisiwa cha Taiwan ambacho China inaona kama sehemu muhimu ya ardhi yake.

"China inaendeleza maendeleo ya amani na jeshi la China linalinda uhuru, usalama na maslahi ya nchi," amesema Waziri wa Ulinzi wa China.

Jim Mattis, Waziri wa kwanza wa Ulinzi wa Marekani kutembelea China tangu mwaka 2014, amesema mazungumzo yake huko Beijing yanajikita kwa "majadiliano ya wazi na ya uaminifu", kama ilivyokuwa na mwenzake wa Kichina.

Bw Mattis amemuomba Wei kuzuru Pentagon.