Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHINA-USALAMA

Washington yaionya Beijing dhidi ya vita kwenye bahari ya China

Ikulu ya White Haouse imeionya China kwamba inajiweka "hatarini" kuhusu "vita" vyake kwenye bahari ya nchi hiyo, ambapo inadaiwa kuwa China hivi karibuni iliweka makombora, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani.

Srah Sanders, msemaji wa serikali ya Marekani.
Srah Sanders, msemaji wa serikali ya Marekani. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

"Tunafahamu vizuri nia ya China kutaka kuzorotesha usalama kwenye bahari iliyo kusini mwa nchi hiyo," msemaji wa serikali ya Marekani Sarah Sanders amesema.

"Tumeelezea wasiwasi wetu kuhusu swala hili moja kwa moja kwa China na kutakuwa na madhara ya muda mfupi na ya muda mrefu," msemaji wa serikali ya Marekani amesema, bila kufafanua madhara hayo.

China imekataa kuthibitisha taarifa zilizotolewa siku ya Jumatano wiki hii na kituo cha televisheni cha CNBC, taarifa ambazo zinaesem akuwa China iliweka makombora katika visiwa vitatu katika Bahari ya kusini mwa nchi hiyo kwa muda wa siku 30 zilizopita, na hivyo kuiruhusu kuunga mkono madai yake ya uhuru.

China inadai kwa sababu za kihistoria visiwa vingi na miamba ya Bahari ya Kusini ya China ni maeneo yake. Mataifa jirani (Vietnam, Ufilipino Malaysia, Brunei) wana madai kama hayo wakati mwingine huingiliana.

China inaunga mkono madai yake ya uhuru kwa kuimarisha visiwa vya na miamba ambayo inadhibiti. Imekua ikijenga mitambo ya raia na viwanja vya ndege vyenye uwezo wa kupokea ndege za kijeshi.

Washington na nchi nyingine za Magharibi wamesisitiza kuwa migogoro katika eneo hili kubwa la bahari inapaswa kutatuliwa kisheria na uhuru wa usafiri unapaswa kuheshimiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.