Pata taarifa kuu
CAMEROON-UN-MAUAJI-USALAMA

Mauaji Cameroon: Umoja wa Mataifa watoa wito kwa serikali kuanzisha uchunguzi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasema amesikitishwa na taarifa kuhusu mauaji ya raia ikiwa ni mapoja na watoto yaliyotokea katika kijiji cha Ngarbuh Februari 14, Kaskazini Magharibi mwa Cameroon, eneo linalozungumza Kiingereza.

Mnara wa muungano wa Cameroon, huko Yaoundé.
Mnara wa muungano wa Cameroon, huko Yaoundé. Wikimédia/Z.NGNOGUE
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari, watu 22 waliuawa Ijumaa asubuhi kwenye kijiji cha Ngarbuh.

Kupitia msemaji wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito kwa serikali ya Cameroon kuanzisha uchunguzi na kuchukua hatua muhimu ili wahusika wajibu walichokifanya.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa rambi rambi zake kwa familia za wahanga."

"Katibu Mkuu ametoa wito kwa pande zote zinazokinzana kujizuia na shambulio lolote dhidi ya raia na kuheshimu sheria za kimataifa zihusuzo haki za binadamu na haki za binadamu," ameongeza msemaji wake.

Shambulio katika kijiji cha Ngarbuh lilitokea katika hali ya mvutano mkubwa iliyokua katika majimbo yanayozungumza Kiingereza Kaskazini-Magharibi na Kusini-Magharibi mwa Cameroon.

Bw Guterres amesisitiza utayari wa Umoja wa Mataifa kufanya kazi na wadau wote kupata suluhisho la kisiasa la mzozo katika majimbo hayo kupitia mazungumzo.

Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR), takriban wakimbizi 8,000 wa Cameroon wamekimbilia Magharibi na kusini mwa Nigeria katika majimbo ya Taraba na Cross Rivers ndani ya kipindi cha wiki mbili zilizopita, na idadi hii imetimiza wakimbizi kutoka Cameroon kufikia 60,000 nchini Cameroon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.