Pata taarifa kuu
CAMEROON-MAUAJI-USALAMA

Ishirini na mbili waangamia katika shambulio Ntumbo, Cameroon

Watu ishirini na wawili, ikiwa ni pamoja na watoto 14, wameuawa Kaskazini Magharibi mwa eneo linalozungumza Kiingereza nchini Cameroon.

Askari wakipiga doria Bafut, Kaskazini-Magharibi mwa Cameroon, katika eneo linalozungumza Kiingereza, Novemba 15, 2017.
Askari wakipiga doria Bafut, Kaskazini-Magharibi mwa Cameroon, katika eneo linalozungumza Kiingereza, Novemba 15, 2017. AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, watoto kumi na wanne, ikiwa ni pamoja na watoto tisa walio na umri ulio chini ya miaka mitano, ni miongoni mwa wahanga wa mauaji hayo.

Ukatili huo ulitekelezwa siku ya Ijumaa wiki iliyopita, katika kijiji cha Ntumbo, Kaskazini-Magharibi mwa eneo linalozungumza Kiingereza. "Kulingana na taarifa ambayo imethibitishwa, raia ishirini na mbili waliuawa asubuhi ya Februari 14. Watu wenye silaha, kwa sababu zisizojulikana, wamewalenga raia hawa. Kati ya wahanga ishirini na mbili (…), kumi na nne walikuwa watoto. Na tunaamini kuwa tisa kati yao walikuwa na imri ulio chini ya miaka mitano. Kulingana na ushahidi tunao, wengi walipigwa risasi na miili yao ilichomwa moto katika nyumba zilizoteketezwa kwa moto. Tunajua pia kuwa mmoja wa wahanga, mwanamke, alikuwa mjamzito. Mwanamke mwengine mjamzito alipigwa risasi na kujeruhiwa. Kwa bahati nzuri, bado yuko hai. Amelazwa hospitalini na yuko katika hali mbaya. Lakini, mtoto tumboni alifariki, ", ameiambia RFI, James Nunan, Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu, OCHA katika majimbo ya Kaskazini-Magharibi na Kusini-Magharibi, Maeneo mawili yanayozungumza Kiingereza.

Wakili Félix Agbor Mballa, mmoja wa viongozi wa maandamano katika maeneo yanayozungumza Kiingereza na mkuu wa shirika moja la haki za binadamu, amelaani "mauaji ya kutisha" ya watoto na wanawake katika kitongoji hicho kinachojulikana kwa jina la Ngarbu. Ametoa wito kwa mamlaka kuanzisha uchunguzi ili kubaini waliohusika na uhalifu huo.

"Uchunguzi unapaswa kufanywa na wajumbe wa asasi za kiraia, serikali na upinzani, hilo ni jukumu la sote. Lazima tujue ni nani aliyefanya hivi na lazima tupate suluhisho la vita hii isiyo na maana. Raia ndio wanaathiriwa. Ni jambo la kusikitisha kwa kile kinachoendelea kati ya watu wanaotaka maeneo yao kujitenga na serikali, " ameongeza Wakili Félix Agbor Mballa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.