Pata taarifa kuu
MAZUNGUMZO-AMANI

Juba na makundi yaliokataa kusaini mkataba wa amani wa 2018 waanza mazungumzo

Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sudan Kusini na makundi yaliokataa kusaini mkataba wa amani wa 2018, ili kuimarisha hali ya kisiasa na usalama, yameanza rasmi jijini Nairobi.

Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir huko Juba, Februari 3, 2023.
Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir huko Juba, Februari 3, 2023. AP - Gregorio Borgia
Matangazo ya kibiashara

Rais Salva Kiir amesema upande wa serikali umekuja kwenye mazungumzo hayo kwa nia njema ya kupata suluhu.

Mweneyekiti wa mkutano huo, William Ruto amesema nchi yake itasimama na Sudan Kusini hadi suluhu itakapopatikana.

Kenya ambayo ni mshirika wa karibu wa Sudan Kusini, iliiongoza pia kwenye mazungumzo ya awali yaliyozaa taifa hilo lililojitenga na Sudan mwaka 2011 lakini limeendelea kushuhudia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.