Pata taarifa kuu

Mali : Wanajihadi na makundi ya kikabili yamewaua raia 45 : HRW

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch, linayatuhumu makundi ya wanajihadi wa kiislamu na wale kutoka makundi ya kikabila nchini Mali kwa kuhusika na mauaji ya raia takribani 45, katika mashambulio tofauti ya mwezi Januari mwaka huu, katikati mwa nchi hiyo.

Serikali ya Mali imekuwa ikikabiliana na makundi ya watu wenye silaha nchini humo, wengi wakiwa wanahusishwa na kundi la Al-Qaeda.
Serikali ya Mali imekuwa ikikabiliana na makundi ya watu wenye silaha nchini humo, wengi wakiwa wanahusishwa na kundi la Al-Qaeda. © OLYMPIA DE MAISMONT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo, Wapiganaji wenye uhusiano na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda, waliua raia zaidi ya 32, pamoja na kuchoma moto nyumba zaidi ya 300 katika vijiji cha Ogota na Ouembe, januari 27.

Aidha katika mwezi huohuo, wapiganaji wanajiita Dozo kutoka jamii ya Bambara ambao wengi ni wawindaji, waliua raia 13 na kuwateka wengine zaidi ya 24 katika vijiji cha Boura na Kalala, ambavyo vinakaliwa na jamii ya watu wa Fulani.

Tangu mwaka wa 2012, Mali imekuwa ikikumbwa na vitendo vya makundi yenye mafungamano na Al-Qaeda na Islamic State, ghasia zinazofanywa na makundi yaliyotangaza kujilinda na ujambazi.
Tangu mwaka wa 2012, Mali imekuwa ikikumbwa na vitendo vya makundi yenye mafungamano na Al-Qaeda na Islamic State, ghasia zinazofanywa na makundi yaliyotangaza kujilinda na ujambazi. © AFP

Katika taarifa yake, shirika hilo limeongeza kuwa mauaji hayo ni sawa na uhalifu wa kivita.

Eneo la katikati mwa nchi ya Mali, limekuwa kitovu cha machafuko tangu mwaka 2015, baada ya kuanza kwa uasi wa makundi ya kijihadi na kuibuka kwa kiongozi wa kabila la Fulani, Amadou Koufa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.