Pata taarifa kuu

Kenya : Wadau wa kilimo wanajadili mbinu zinazoweza kuwasaidia wakulima Afrika

Kwenye kongamano la kujadili ubora wa udongo na mbolea barani Afrika, linalofanyika jijini Nairobi Mawaziri wa Kilimo wamekutana kujadili mbinu zinazoweza kuwasaidia wakulima.

Kongamano hili linatarajiwa kukamilika hii leo Alhamis jijini Nairobi Nchini Kenya.
Kongamano hili linatarajiwa kukamilika hii leo Alhamis jijini Nairobi Nchini Kenya. © AU
Matangazo ya kibiashara

Wadau mbalimbali kutoka barani Afrika wamekuwa wakikutana kwa siku tatu sasa kujadili masuala ya umuhimu kuhusiana na kilimo bora katika ukanda wa Afrika.

Lusebia Abdulilahi ni waziri wa kilomo nchini Nigeria.

‘‘kwa sasa tuna mikakati ya kuzindua mpango wa afya ya udongo kwa wakulima, ili kuwapa ushauri wakulima kwa kile wanahitaji kukifanya kuwa na udongo wenye rotuba, kwa hivyo mkutano huu ni muhimu kwetu.’’ alisema Lusebia Abdulilahi ni waziri wa kilomo nchini Nigeria.

00:13

Lusebia Abdulilahi ni waziri wa kilomo nchini Nigeria

Mbinu hizo ni pamoja na kuongeza virutubishi na madini hai kwenye udongo, kuhakikisha uwepo wa mbefu safi. Emanile Chauka ni waziri wa kilimo wa Eswatini.

‘‘Lengo letu ni kuhakikisha tumeimarisha matumizi ya mbolea bora, kuongeza mazao, lakini pia tuhakikishe tunatunza rutuba ili kuwepo na afya nzuri ya udongo, si kwa ajili yetu tu bali kwa maendeleo pia.’’ alieleza Emanile Chauka ni waziri wa kilimo wa Eswatini.

00:18

Emanile Chauka ni waziri wa kilimo wa Eswatini

Naye, Josefa Sacko, kamishena wa kilimo katika umoja wa Afrika, ameyataka mataifa ya Afrika kuzingatia ushirikiano na sekta mbalimbali mbali za kilimo ili kuafikia malengo yaliyowekwa baada ya kongamano hili.

‘‘Nawahimiza mawaziri waamue na pia tufanye kazi na washirika ilituzifanyie kazi agenda zilizoekwa.’’ Walisema baadhi ya wadau wanaohudhuria kongamano hili.

00:27

Wadau katika sekta ya kilimo barani Afriika

Kongamano hili linatarajiwa kukamilika hii leo Alhamis jijini Nairobi Nchini Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.