Pata taarifa kuu
CAMEROON-USALAMA

Cameroon: Meli ya mafuta ya Ugiriki yashambuliwa, mabaharia wanane watekwa nyara

Meli ya mafuta ya Ugiriki imeshambuliwa na watu wenye silaha. Wafanyakazi wanane kati ya 28 wametekwa nyara, raia watano wa Uigiriki ni miongoni mwa mateka hao, ikiwa ni pamoja na nahodha wa meli.

Vikosi vya jeshi la Marekani, Afrika na Ulaya wakati wa zoezi la kimataifa lenye lengo la kuimarisha usalama wa baharini katika Ghuba ya Guinea, mwaka 2014.
Vikosi vya jeshi la Marekani, Afrika na Ulaya wakati wa zoezi la kimataifa lenye lengo la kuimarisha usalama wa baharini katika Ghuba ya Guinea, mwaka 2014. © U.S. Navy cc Jeff Atherton
Matangazo ya kibiashara

Wafilipino wawili na raia mmoja wa Ukraine pia wametekwa nyara. Tukio hilo lilitokea Jumanne Desemba 31 kwenye bandari ya Limbe.

Waziri wa Uigiriki wa Jeshi la Majini, Yannis Plakiotakis, ameandika kwenye mtandao wa Facebook kwamba anaendelea kufikiria hatma ya mabaharia wanaoshikiliwa kinyume cha sheria na kufikiria pia familia zao. Amesema pia kuwa serikali ya Ugiriki inafanya kilio chini ya uwezo wakeili mabaharia hao waweze kuachiliwa na kurudi nyumbani.

Wakati wa shambulio hilo, meli inayojulikana kwa jina la Happy Lady ilikuwa kwenye pwani ya Limbe, moja ya bandari kuu za Cameroon. Wakati wa shambulio hilo, mhandisi wa meli hiyo ya mafuta ya Uigiriki pia alijeruhiwa kwa risasi, lakini hali yake si mbaya, kwa mujibu wa vyanzo vya hospitali.

Hata hivyo wahusika nchini Cameroon bado hawajathibitisha kadhia hiyo inayoaminika kuwa ya tatu ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Mwezi Novemba meli nyingine ya mafuta ya Ugiriki inayojulikana kwa jina la Elka Aristotle, ilishambuliwa wakati ilikuwa imeegeshwa katika pwani ya Lome, mji mkuu wa Togo. Wakati huo mabaharia wanne walitekwa nyara. Watatu kati yao waliachiliwa katikati ya mwezi Desemba, lakini wa nne alifariki dunia akiwa mikononi mwa watekaji nyara.

Matukio haya ya uharamia yamekuwa sugu kwenye Ghuba ya Guinea ambayo inaanzia kusini mwa Senegal hadi Angola. Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la usalama wa majini (BMI), visa hivi vilianza kuongezeka mnamo mwaka 2017. Na vinashuhudiwa katika nchi zaidi ya kumi.

Mnamo mwezi Desemba pekee, matukio matatu yaliripotiwa. Desemba 3, mabaharia 19 walitekwa nyara katika pwani ya Nigeria, mabaharia 20 walitekwa nyara Desemba 15 katika pwani ya Benin. Desemba 21 meli nne zilishambuliwa kwenye pwani ya Libreville, nchini Gabon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.