Pata taarifa kuu

Ndege yakosea njia kwenye uwanja wa ndege wa Dakar, kumi na moja wajeruhiwa

Watu 11 wamejeruhiwa leo Alhamisi, wanne kati yao vibaya, wakati ndege aina ya Boeing iliyokodishwa na Air Senegal ilipokosea njia wakati ilipokuwa ikijaribu kuruka, tukio ambalo lilisababisha kufungwa kwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Diass, karibu na Dakar, umetangaza uongozi wa wanja huo.

Tukio hilo limesababisa " watu kumi na mmoja kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wanne ambao wamejeruhiwa vibaya" kati ya abiria 78.
Tukio hilo limesababisa " watu kumi na mmoja kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wanne ambao wamejeruhiwa vibaya" kati ya abiria 78. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo aina ya B737/300, iliyokodishwa kutoka kwa kampuni ya kibinafsi, Transair, ikiondoka kuelekea Bamako, "ilitoka kwenye njia yake ya kuruka wakati ilipokuwa ikiruka Alhamisi hii, Mei 9, 2024 karibu saa 7:00 usiku," imesema idara ya mawasiliano ya mamlaka ya wa uwanja wa ndege katika taarifa.

Tukio hilo limesababisha "watu kumi na mmoja kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wanne ambao wamejeruhiwa vibaya" kati ya abiria 78, anasema meneja wa mamlaka ya uwanja wa ndege, ambaye anabainisha kuwa uwanja wa ndege "umefungwa kwa sasa wakati wakisubiri mipango iliyopangwa kufanywa". Abiria wengine sita wamelazwa kwa uangalizi katika huduma za matibabu katika uwanja wa ndege, kulingana na chanzo hicho.

"Kufunguliwa tena kwa uwanja wa ndege kutatangazwa katika saa zijazo," imeongeza mamlaka ya uwanja wa ndege.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.