Pata taarifa kuu
DRC-MGOMO-AFYA

Madai ya madaktari kupatiwa ufumbuzi DRC

Mazungumzo baina ya serikali ya Jamuhuri ya Kimdekokrasia ya Congo na madaktari waliopo mgomoni yanaendelea wakati huu madatkari wakiwa na matumaini ya kupatikana kwa muafaka baada ya serikali kuonekana kulivalia njuga swala lao.

Hopitali Panzi mjini Bukavu, mashariki mwa DRC, Julai 2014.
Hopitali Panzi mjini Bukavu, mashariki mwa DRC, Julai 2014.
Matangazo ya kibiashara

Madaktari hao wanaojumuika katika shrika la CINAMED wanaodai kulipta malimbikizo ya mishahara yao na mabadiliko ya viwango vya mshahara wa madaktari na kulipwa viinuwa mgongo

Mazungumzo hayo yana simamiwa na waziri mkuu wa serikali Bruno Tshibala na kulingana na Dokta John Sanga katibu mkuu wa shirika linalo tetea haki za madaktari kuna maendeleo chanya baada ya serikali kutowa mapendekezo yanayo ridhisha.

Mazungumzo yanaendelea hii leo ijumaa baina ya pande hizo mbili ambapo hii leo kwenye wizara ya bajeeti wanajadili kuhusu kile kinachowezekana katika mapendekezo yaliotolewa na madaktari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.