Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Polisi yawatawanya wafuasi wa upinzani nchini Zimbabwe licha ya mahakama kuwaruhusu

Polisi wa kutuliza ghasia nchini Zimbabwe wametumia mabomu ya machozi, risasi za mpira, kuwapiga waandamanaji na kuwazuia kukusanyika kwenye uwanja ambao muungano wa upinzani nchini humo unao fahamika kama NERA ulikuwa ufanye mkutano jijini Harare.

Baadhi ya raia wakiwa wanakimbia baada ya kuanza kukabiliana na Polisi jijini Harare, Zimbabwe, 26 Agosti, 2016
Baadhi ya raia wakiwa wanakimbia baada ya kuanza kukabiliana na Polisi jijini Harare, Zimbabwe, 26 Agosti, 2016 DR
Matangazo ya kibiashara

Maandamano haya ambayo yameruhusiwa na mahakama kuu, yalilenga kupinga kufanyika kwa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2018, ambapo rais wa sasa Robert Mugabe anatarajiwa kuomba kuchaguliwa tena.

Mwakilishi wa Radio France International aliyeko nchini Zimbabwe, amesema kuwa ameshuhudia polisi wakitumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya waandamanaji waliokuwa tayari wameanza kukusanyika kwenye uwanja maarufu wa Robert Mugabe jijini Harare.

Hata hivyo mkusanyiko uliokuwa wa amani uligeuka kuwa vurugu baada ya waandamanaji kuamua kuwarushia mawe Polisi waliokuwa wakiwatawanya huku magari na mali kadhaa zikiharibiwa.

Mamia ya wananchi waliokuwa wamekusanyika kwenye uwanja huo, walianza kurusha mawe kulenga magari ya raia wa kawaida na yale ya Serikali huku waking’oa mabango yenye picha na maandishi yanayolitaja jina la Rais Mugabe.

Polisi wanasema walikuwa hawajapokea hukumu ya mahakama iliyokuwa inaruhusu kufanyika kwa maandamano hayo ndio maana waliamua kuchukua jukumu la kuwatawanya waandamanaji hao.

Kwenye uamuzi wake, mahakama kuu imesema suala la kuandamana na kufanya mikutano ni suala la kikatiba, ambapo aliruhusu maandamano hayo ya upinzanik kuanza kufanyika kuanzia saa sita mchana hadi saa kumi jioni, na kuagiza Polisi kutoa ulinzi kwa waandamanaji.

Msemaji wa chama cha MDC, Douglas Mwanzora, amesema hukumu ya mahakama wameichukulia kama ushindi kwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.