ZIMBABWE-MAANDAMANO
Maandamano ya upinzani yatawanywa Zimbabwe
Polisi ya Zimbabwe imetumia mabomu ya machozi na mizinga ya maji kwa kuwatawanya waandamanaji dhidi ya serikali.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Karibu waandamanaji 200 wameshutumu kile walichokiita ukatili wa polisi na kutoa wito kwa Rais Robert Mugabe kujiuzulu.
Vyama vya upinzani nchini Zimbabwe vimepanga kufanya maandamano ya pamoja Ijumaa wiki hii mjini Harare.
Maandamano dhidi ya serikali yameongezeka dhidi ya sera za kiuchumi za Rais Robert Mugabe.
Zimbabwe imeachana na sarafu yake ya kitaifa baada ya kukumbwa na mfumuko wa bei kwa asilimia bilioni mwaka 2009.
Mugabe anaongoza Zimbabwe kimabavu tangu nchi hiyo kupata uhuru wake mwaka 1980.