Pata taarifa kuu
DRC-UPINZANI-SHERIA-SIASA

DRC: Mbunge Martin Fayulu akamatwa kisha aachiwa

Kwa mujibu wa mashahidi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mmoja wa wapinzani wakuu, Mbunge Martin Fayulu, amekamatwa mapema Jumapili hii mchana kwenye makao makuu ya chama chake mjini Kinshasa.

Martin Fayulu (kulia) baada ya kuachiwa Jumapili hii, Februari 14, 2016, akiambatana na mpinzani Kamerhe (kushoto).
Martin Fayulu (kulia) baada ya kuachiwa Jumapili hii, Februari 14, 2016, akiambatana na mpinzani Kamerhe (kushoto). © RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa chama cha ECIDE, akiwa pia mjumbe wa muungano wavyama vya upinzani na mgombea urais, Martin Fayulu aliwatolewa wito wafuasi wake kususia shughuli mbalimbali Februari 16 akidai kudai uchaguzi ufanyike ndani ya muda uliopangwa kikatiba, kuheshimu Katiba na kanuni za kupishana madarakani kidemokrasia.

Mbunge Martin Mayulu alirudishwa nyumba kwake chini ya ulinzi mkali baada ya kuzuiliwa kwa saa kadhaa, licha ya kuwa na kinga ya ubunge. Martin Fayulu alikamatwa akiwa kwenye makao makuu ya chama chake kwa minajili ya maandalii ya kampeni ya kuhamasisha wafuasi wake kuhusu maandamano ya siku ya Jumanne wiki hii. Mbunge huyo wa upinzani ameiambia RFI kwamba alikamatwa katika mazingira ya vurugu na.

Baada ya kupelekwa katika ofisi za Idara ya upelelezi wa kijeshi, Martin Fayulu hatimaye alipewa fursa ya kukutana na mwanasheria wake. Msemaji wa serikali alitangaza kuachiliwa kwake kwenye majira ya saa 2:30 usiku saa moja baada ya kuzuiliwa.

Kwa mujibu wa Lambert Mende, Martin Fayulu alikamatwa kwa kosa la kuchochea vurugu. "Mara baada ya kutambuliwa kama mbunge na afisa wa ofisi ya mashitaka, aliachiliwa mara moja", Waziri wa Mawasiliano amesema, akibaini kwamba "faili imefunguliwa, hatua ambayo ambayo itafuata ni kuona iwapo Bunge litafanyia kazi suala hili, kwani vyombo vya sheria vinapaswa kusubiri idhini ya Bunge ili kuweza kufuatilia mbunge Marin Fayulu. "

Maoni

Mjumbe maalum wa Marekani katika Ukanda wa Maziwa Makuu ameelezea wasiwasi wake baada ya kukamatwa kwa Mbunge Fayulu. "Kuwatuhumu wapinzani kuwa ni wahalifu kunawezakuzua vurugu",Tom Perriello amelaumu kwenye Twitter.

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu anaona kuwa "kumkamata kiongozi wa upinzani ni hatua kubwa zaidi inayothibitisha kwamba nafasi ya kisiasa inaendelea kudorora na kuna ukiukwaji wa haki na uhuru nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. "

Kwa upande wake Ida Sawyer, mkuu wa shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesema kukamatwa kwa Mbunge huyo ni ishara inayotia wasiwasi. "Hii ni kesi ya mwisho ya ukandamizaji dhidi ya wapinzani na wanaharakati wa mashirika ya kiraia wanaoomba kuheshima muda uliopangwa kikatiba katika maandalizi ya uchaguzi", amesema na kuongeza kuwa ni kesi moja miongoni mwa nyingi zilioorodheshwa na shirika lake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.