Pata taarifa kuu
DRC-UPINZANI-SHERIA-SIASA

DRC: Mbunge wa upinzani Martin Fayulu akamatwa

Kwa mujibu wa mashahidi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mmoja wa wapinzani wakuu, Mbunge Martin Fayulu, amekamatwa mapema Jumapili hii mchana kwenye makao makuu ya chama chake mjini Kinshasa.

Mbunge Martin Fayulu.
Mbunge Martin Fayulu. © CC/Mclums
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa chama cha ECIDE, akiwa pia mjumbe wa muungano wavyama vya upinzani na mgombea urais, Martin Fayulu aliwatolewa wito wafuasi wake kususia shughuli mbalimbali Februari 16 akidai kudai uchaguzi ufanyike ndani ya muda uliopangwa kikatiba, kuheshimu Katiba na kanuni za kupishana madarakani kidemokrasia.

Msemaji wa serikali, Lambert Mende amethibitisha kukamatwa kwa mwanasiasa huyo. Martin Fayulu amesikilizwa na afisa wa ofisi ya mashitaka, ambert Mende amesea bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi. Waziri huyo wa Mawasiliano wa Congo ameongeza kwamba Martin Fayulu ni mbunge, anapaswa kuachiwa huru.

Kwa upande wake Ida Sawyer, mkuu wa shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesema kukamatwa kwa Mbunge huyo ni ishara inayotia wasiwasi. "Hii ni kesi ya mwisho ya ukandamizaji dhidi ya wapinzani na wanaharakati wa mashirika ya kiraia wanaoomba kuheshima muda uliopangwa kikatiba katika maandalizi ya uchaguzi", amesema na kuongeza kuwa ni kesi moja miongoni mwa nyingi zilioorodheshwa na shirika lake.

Itakumbukwa kwamba, vyama vingi vya upinzani pamoja na vyama vya kiraia wanaishtumu serikali na tume ya uchaguzi kwamba wanatafuta kulazimisha kusogezwa mbele kwa kalenda ya uchaguzi kwa kumruhusu Joseph Kabila, ambaye anamaliza muhula wake wa pili kikatiba kubaki madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.