Pata taarifa kuu

Kandanda: Shoka nyingine tena kwa timu ya Everton

Everton yapunguziwa pointi mbili kwa kukiuka kwa mara ya pili kanuni za fedha za Ligi Kuu nchini Uingereza

Uwanja wa Everton Goodison Park
Uwanja wa Everton Goodison Park AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Timu inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza Everton imepokonywa pointi mbili kwa kukiuka mara ya pili kanuni za fedha za Ligi hiyo.

Sheria za faida na uendelevu (PSR) ziliruhusu vilabu kupoteza pauni milioni 105 kwa miaka mitatu na tume huru ilipata Everton imekiuka hilo kwa pauni milioni 16.6 kwa kipindi cha miaka mitatu hadi 2022-23.

Hatua hii inamaanisha kuwa Everton itashuka nafasi moja hadi ya 16 na sasa wako pointi mbili juu ya eneo la kushushwa daraja.

Toffees ilipunguziwa pointi 10 hadi sita baada ya kukata rufaa mwezi Februari kwa kipindi cha miaka mitatu hadi 2021-22.

Everton imesema klabu hiyo itakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Katika sababu zake zilizoandikwa tume huru ilikubali hoja za klabu za kupunguza kuhusiana na ukweli ambao klabu:

  • Tayari imepunguziwa pointi msimu huu
  • Kupoteza mapato ya klabu kwa sababu ya kusitishwa kwa mkataba wa udhamini na kampuni ya Urusi ya USM
  • Kukiri hatia mapema
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.