Pata taarifa kuu
UINGEREZA-CHINA-HAKI

Polisi: Miili ya watu 39 iliopatikana katika kasha la lori walikuwa Wachina

Polisi ya Uingereza imethibitisha kwamba milii ya watu 39 iliopatikana katika kasha la gari ya mizigo katika mji wa Essex, nchini Uingereza walikuwa raia wa China.

Polisi wakichunguza miili 39 iliyopatikana Grey katika mji wa Essex.
Polisi wakichunguza miili 39 iliyopatikana Grey katika mji wa Essex. REUTERS/Peter Nicholls
Matangazo ya kibiashara

China imetangaza kwamba wafanyakazi wa ubalozi wake wako njia wakielekea London ili kuhakikisha habari hiyo.

Wakati huo huo, wachunguzi wanaendelea kuchunguza nchi ambayo lori hilo lilitokea, na wamebaini kwamba gari hilo linaweza kuwa lilitokea Ireland ya Kaskazini au Ubelgiji.

Kasha la gari ya mizigo ambalo lilikuemo miili hiyo ya watu 39 liliwasili usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano wiki hii katika bandari ya Purfleet kwenye Mto wa Thames, likitokea Zeebrugge nchini Ubelgiji.

Lori hilo ambalo liliegesha kasha (kontena) hilo lilikuwa tayari limerudi Ireland ya Kaskazini, ambapo dereva wa miaka 25 aliyekamatwa kwa uchunguzi wa mauaji, ni raia wa nchi hiyo.

Msako uliendeshwa jana Jumatano katika nyumba tatu katika Kaunti ya Armagh, ambapo kijana huyo anaishi, wakati polisi inajaribu kutambua genge la wahalifu ambalo linaweza kuwa linahusika na uhalifu huo.

Kwa upande wake, mamlaka nchini Ubelgiji pia imefungua uchunguzi kuhusu waandaaji wa biashara hiyo na washiriki wao. Msemaji wa mamlaka hiyo amsema lori hilo liliwasili Zeebrugge karibu saa 8:30 mchana Jumanne Oktoba 22 na kuondoka bandarini alasiri.

Haijulikani ikiwa waathiriwa walianzia safari yao nchini Ubelgiji au katika nchi nyingine. Polisi imethibitisha kwamba watu hao walikuwa raia wa China, wanawake 8 na wanaume 31, na sasa inajaribu kuchunguza mazingira vifo vyao na wakati waliofariki dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.