Pata taarifa kuu
FIFA-UFISADI

Wachunguzi wa FIFA kukata rufaa kwa uamuzi dhidi ya Blatter na Platini

Wachunguzi wa shirikisho la Soka Duniani (FIFA), ambao walipinga uamuzi wa kufukuzwa moja kwa moja dhidi ya Michel Platini na Joseph Blatter, wametangaza Jumanne hii nia yao ya kukata rufaa ya kusimamishwa kwa muda wa miaka 8 kwa viongozi hao katika shughuli ya aina yoyote inayohusiana na soka.

Rais wa UEFA Michel Platini (kulia) na rais wa FIFA Sepp Blatter baada ya uchaguzi wa Blattter, katika kutano mkuu wa Shirikisho la FIFA, Zurich, Mei 29, 2015.
Rais wa UEFA Michel Platini (kulia) na rais wa FIFA Sepp Blatter baada ya uchaguzi wa Blattter, katika kutano mkuu wa Shirikisho la FIFA, Zurich, Mei 29, 2015. REUTERS/Arnd Wiegmann
Matangazo ya kibiashara

"Kitendo cha Uchunguzi cha FIFA kinatarajia kuanzisha utaratibu wa kukata rufaa dhidi ya uamuzi uliyotolewa dhidi ya Joseph Blatter na Michel Platini kwa Kamati ya Rufaa ya FIFA", amesema katika tangazo alilotuma kwenye shirika la habari la Ufaransa AFP, Andreas Bantel, msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi na Tume ya Maadili ya FIFA ; Mahakama ya ndani ya taasisi kuu ya soka.

Mahakama hii inaundwa na vitengo viwili: Kitengo cha Uchunguzi, ambacho kinaundwa kwa upande wake na wachunguzi ambao ni waendesha mashitaka, waliopinga uamzi wa kuwafuta moja kwa moja Joseph Blatter na Michel Platini; na Kitengo cha Hukumu, kilichochukua uamzi wa kuwasimamisha viongozi hao kwa kipindi cha miaka minane.

Ni wazi kuwa, majaji wa FIFA walioendesha uchunguzi wanaona kuwa kashfa ya rushwa ambayo iliondolewa katika mashtaka dhidi Mswisi, mwenye umri wa miaka 79 na Mfaransa mwenye umri wa miaka 60, inapaswa kuzingatiwa.

"Hakukuwa na ushahidi wa rushwa na kitengo cha hukumu kiliona kuwa shutma hiyo haina msingi", wanasheria wa Blatter wamesema katika taarifa iliyotumwa kwenye shirika la habari la Ufaransa AFP. Baadhi ya wajumbe wa Kitengo cha Uchunguzi walifutilia mbali shutma hiyo kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha.

Mahakimu wa FIFA ambao walitangaza uamuzi dhidi ya viongozi hao wa soka duniani Desemba 21 na waliweka mbele makosa ya "utumiaji mbaya wa madaraka" na "mgogoro wa maslahi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.