Pata taarifa kuu
REAL MADRID-ZIDANE-SOKA

Soka: Zidane ateuliwa kuwa kocha wa Real Madrid

Real Madrid imemteua Jumatatu hii Januari 4, 2016 Zinedine Zidane kuwa kocha wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Mhispania Rafael Benitez.

Mfaransa Zinédine Zidane.
Mfaransa Zinédine Zidane. AFP PHOTO / GERARD JULIEN
Matangazo ya kibiashara

"Zidane kuanzia sasa ni kocha mpya wa Real Madrid na kwa mimi ni furaha tele", amesema Rais wa Real, Florentino Perez, katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu hii jioni mjini Madrid mbele ya Zidane akizungukwa na mke na watoto zake.

Kwa mara ya kwanza ya uzoefu wake mkubwa wa kiufundi, nyota huyu wa soka nchini Ufaransa atainoa klabu hiyo ya Uhispania ambayo inakabiliwa na matatizo chungu nzima msimu huu.

Huu ni mkakati uliyopitishwa na Real Madrid, Jumatatu hii Januari 4, 2016. Klabu hii ya Uhispania imeamua kumfukuza kocha wake Rafael Benitez na nafasi yake ikachukuliwa na Zinedine Zidane.

Mfaransa huyo, mwenye umri wa miaka 43, ambaye aliichezea Real Madrid tangu mwaka 2001 hadi 2006, amaekua akiinoa klabu ya Castilla tangu Juni 2014. Zidane anachukua nafasi ya Benitez, ambaye kamwe klabu yake haikuweza kupata ushindi, tangu uteuzi wake mwezi Juni 2015.

Pamoja na uzowefu wake, kocha wa zamani wa klabu ya Valencia (Uhispania), Liverpool, Chelsea (Uingereza), Inter Milan na Napoli (Italia), alikuwa ametengwa na wachezaji wengi wa Real Madrid.

Zinedine Zidane akiwasili katika mkutano na wanahabari wa rais Florentino Perez wa Real Madrid (kulia) akimteuwa kama kocha wa Real Madrid, Januari 4, 2016.
Zinedine Zidane akiwasili katika mkutano na wanahabari wa rais Florentino Perez wa Real Madrid (kulia) akimteuwa kama kocha wa Real Madrid, Januari 4, 2016. AFP PHOTO/ GERARD JULIEN

Thuram: "ni mtu ambaye ana uongozi"

Watu wengi wamekua wakijiuliza maswali iwapo Zinedine Zidane ataweza kuheshimiwa na Mreno Cristiano Ronaldo na washirika wake? Lilian Thuram, ambaye alishinda Kombe la Dunia la mwaka 1998 na kiungo wa zamani, anaona kuwa Zidane ni kocha mwenye uzoefu mkubwa, na wachezaji wa klabu ya Real Madrid watashirikiana naye vya kutosha.

Kama mchezaji, Zidane alishinda Ligi kuu ya Uhispania (La Liga) mwaka 2003 na hasa Ligi ya Mabingwa 2002. Ligi kuu ya Uhispania na Kombe la Ulaya ni malengo mawili makuu ya "Merengues" (jina la utani la wachezaji wa Real Madrid). Lakini kwa mechi yake ya kwanza kama kocha, Real Madrid hapaswi kutarajia mengi kutoka kwa "Zizou".

"Nataka kuishukuru klabu kwa kunipa nafasi ya kuinoa (....) klabu bora duniani", amesema Zinedine Zidane, mpaka sasa kocha wa ziada, wakati wa hotuba fupi kwa vyombo vya habari baada tu ya tangazo la uteuzi wake. "Mimi najaribu kujiweka sawa", Zidane ameongeza.

Zinedine Zidane, kocha mpya wa Real Madrid akizungukwa na mke wake, watoto zake wanne, na rais wa Real Madrid, Florentino Perez, Januari 4, 2016.
Zinedine Zidane, kocha mpya wa Real Madrid akizungukwa na mke wake, watoto zake wanne, na rais wa Real Madrid, Florentino Perez, Januari 4, 2016. AFP PHOTO/ GERARD JULIEN

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.