Pata taarifa kuu
SOKA-UEFA-JUVENTUS-REAL MADRID

Real Madrid yaangukia pua kwa kufungwa mabao 2-1

Mchuano wa kwanza wa nusu fainali za Kombe la Mabingwa barani Ulaya kati ya Juventus ya Italia na Real Madrid ya Uhispania umechezwa Jumanne usiku wiki hii.

Alvaro Morata (kulia) aliyeipatishia klabu yake ya Juventus bao la kwanza katika dakika ya 8 katika mchuano wa kwanza wa nusu fainali za Kombe la Mabingwa barani Ulaya
Alvaro Morata (kulia) aliyeipatishia klabu yake ya Juventus bao la kwanza katika dakika ya 8 katika mchuano wa kwanza wa nusu fainali za Kombe la Mabingwa barani Ulaya Reuters / Max Rossi
Matangazo ya kibiashara

Hadi dakika 90 za mchezo huo Real Madrid imejikuta imeangukia pua baada ya kufunwa mabao 2-1.
Juventus, ambao walikua wenyeji wa mchuano huo walipata bao la kwanza katika dakika ya 8 ya mchezo kupitia kwa mchezaji Alvaro Morata.

Katika dakika ya 27 ya mchezo, Cristiano Ronaldo alisawazisha na kupelekea timu hizo mbili kwenda sare ya kufungana bao 1 kwa 1 hadi mwisho wa kipindi cha kwanza.

Katika dakika ya 57 Juventus walipata goli la pili, kutokana na mpira wa adhabu ya penalti. Goli ambalo lilifungwa na Carlos Tevez.

Hadi dakika tisini za mchezo, Juventus ilijikuta ikiingiza mabao 2 kwa 1 la Real Madrid . Mchezo wa marudiano utachezwa Mei 13 katika uwanja wa Bernabeu, mjini Madrid.

Michuano ya nusu fainali za Kombe la UEFA itaendelea leo Jumatano , ambapo Barcelona itapimana nguvu na Bayern Munich ya Ujerumani katika uwanja wa Nou Camp.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.