Pata taarifa kuu

Jitihada zarejelewa kupata mwafaka kati ya Israel na Hamas

Mazungumzo yanarejelewa jijini Cairo, kati ya Hamas na Israeli kusitisha vita kwenye ukanda wa Gaza, ambavyo vimekuwa vikiendelea tangu Oktoba mwaka uliopita, licha ya Israeli kusema itashiriki tu iwapo masharti yake yatazingatiwa.

Namna Gaza ilivyoharibiwa na mabomu ya Israeli
Namna Gaza ilivyoharibiwa na mabomu ya Israeli REUTERS - Mahmoud Issa
Matangazo ya kibiashara

Wasuluhishi kutoka Misri, Qatar na Marekani wanaongoza mazungumzo hayo, na yanakuja wakati huu wakisubiri kundi la Hamas kujibu mapendekezo ya Israeli, ya namna ya kusitisha vita.

Kiongozi wa juu wa Hamas, amesema wajumbe wote wamewasili jijini Cairo kwa ajili ya mazungumzo hayo muhimu, huku ripoti kutoka upande wa Palestina, zikisema huenda Hamas wakakubali mkataba wa kusitisha vita.

Ripoti zinasema, Israel imetoa wiki moja kwa kundi la Hamas kukubadili mapendekezo yake, ambayo ni pamoja na kubadilishana wafungwa.

Mazungumzo ya kupata suluhu yalikwama miezi kadhaa iliyopita, kufuatia hatua ya Israeli kuendelea kusisitiza mpango wake wa kuishambulia Rafah na kuupuza shinikizo la Hamas.

Haya yanajiri wakati wiki hii, wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Marekani na Ufaransa wakiandamana na kukabiliana na maafisa wa usalama, kushinikiza kumalizika kwa vita hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.