Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-MALAYSIA-EU-Vikwazo

Ukraine : Umoja wa Ulaya unajadili vikwazo vipya dhidi ya Urusi

Visanduku vya sauti vya ndege ya Malaysia Airlines yenye chama MH17 iliyopata ajali alhamisi Julai 17, vimekabidhiwa juamanne wiki hii wachunguzi kutoka Uholanzi wakati ambapo mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Ulaya wamekua wakikutana mjini Brussels ili kuichukulia vikwazo vipya Urusi.

Frans Timmermans, waziri wa Uholanzi mwenye dhamana ya mambo ya nje, akiwashukuru wenzake wa nchi za Ulaya kwa kunesha mshikamano dhidi ya Moscow.
Frans Timmermans, waziri wa Uholanzi mwenye dhamana ya mambo ya nje, akiwashukuru wenzake wa nchi za Ulaya kwa kunesha mshikamano dhidi ya Moscow. REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo kadhaa vimechukuliwa katika kikao hicho, lakini bado kunaandaliwa vikwazo muhimu. Suala la vikwazo dhidi uuzaji wa silaha bado halijazungumziwa.

Mataifa hayo yanayounda Umoja wa Ulaya yameichukulia Urusi baadhi ya vikwazo lakini vikwazo muhimu bado vinajadiliwa hususn vikwazo katika sekta ya ulinzi na vifaa vingine vya kijeshi na vya kawaida, vikwazo katika sekta ya gesi na mafuta na kutoruhusiwa kuuza bidhaa zake katika masoko ya kimataifa.

Vikwazo hivyo vipya ambavyo bado vinajadiliwa vitaanza kutekelezwa baada ya maombi ya Umoja wa Ulaya ya kuruhusu wataalamu kutoka mataifa mbalimbali kuendesha uchunguzi kwa uhuru kuhusu kuhusu ajali ya ndege ya Malaysia Airlines na kurejea kwa hali ya utulivu katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi nchini Ukraine. Hii ni hatua ya pili kuhusu vikwazo vinavyochukuliwa na mataifa ya Ulaya dhidi ya Urusi, inasalia hatua ya tatu kuhusu vikwazo ambavyo vitaathiri sekta ya uchumi.

Waziri wa Uholanzi mwenye dhamana ya mambo ya nje amewashukuru wenzake kutoa mataifa ya Ulaya kuonesha mshikamano katika kikao hicho na kuonesha pia uungwaji mkono wao mapendekezo yaliyotolewa na Uholanzi juu ya Urusi.

“Mapendekezo ya Uholanzi yamesikilizwa kwa kina, ameseama Frans Timmermans. Ni wazi kwamba hali imebadilika kwa kiwango kikubwa kuhusu kudunguliwa kwa ndege ya Malaysia Airlines. Na ni wazi pia kwamba bado tunashuhudia kwa namna gani Urusi inaunga mkono waasi wanaoshikilia maeneo ya mashariki mwa Ukraine, wakati ambapo silaha zinaingizwa kupitia mpaka wa Urusi na Ukraine kwenye maeneo yanayoshikiliwa na waasi, huku viongozi wa Urusi wakifungia macho jambo hilo. Umoja wa Ulaya ulisema kwamba iwapo hali hii itaendelea, kuna ulazima Urusi ichukuliwe hatua zinazohitajika, hata Uholanzi iliomba iwe hivo”, ameongeza waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi.

Uamzi huu wa Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi ni moja ya vikwazo muhimu vinavyoandaliwa kuchukuliwa. Kuna uwezekano wa kuongeza majina mengine mapya ya viongozi watakaolengwa na vikwazo vya kusafiri na kuziwiliwa mali zao ziliyoko nje ya nchi.

Wakuu wa idara ya ujasusi ya Marekani, wamethibitisha jumanne wiki hii kwamba ndege ya Malaysia Airlines huenda ilidunguliwa bila kukusudiwa na waasi wa Ukraine wanaoungwa mkono na Urusi, ambao hawajapata mafuzo ya kutosha Wakuu hao wametupilia mbali lawama za Urusi dhidi ya Ukraine kwamba ndio ilihusika na udunguaji wa ndege ya Malaysia Airlines.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.