Pata taarifa kuu
IRAQ-KURDISTAN-UHURU-SIASA

Asilimia 93 ya Wakurdi wa Iraq wapiga kura ya "Ndiyo" kwa uhuru

Wakurdi wa Iraq wamepiga kura kwa asilimia 93 kwa uhuru wa eneo lao wakati kura ya maoni ya siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa matokeo ya mwisho ya kura yaliyotangazwa Jumatano hii.

Tume ya Uchaguzi yatangaza matokeo ya kura ya maoni ya uhuru wa Kurdistan nchini Iraq katika mji wa Erbil tarehe 27 Septemba 2017.
Tume ya Uchaguzi yatangaza matokeo ya kura ya maoni ya uhuru wa Kurdistan nchini Iraq katika mji wa Erbil tarehe 27 Septemba 2017. REUTERS/Alaa Al-Marjani
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya asilimia 72 ya wapiga kura walioorodheshwa, sawa na watu milioni 3.3, walishiriki katika kura hiyo ya maoni na kura ya "ndiyo" ilishinda kwa asilimia 92.73 ya kura zilizopigwa, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi na kura ya maoni ya eneo la Kurdistan.

Wapiga kura walitakiwa kupiga kura ya "Ndiyo" au "Hapana" kwa kura hiyo ya maoni.

Swali hapa ilikua kuamua kama eneo la Kurdistan na maeneo ya Kikurdi ya nje ya eneo la Kurdistan kuwa nchi huru."

Serikali ya Iraq inataka kufutwa kwa matokeo ya kura, ambayo inaona kuwa ni kinyume na katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.