Pata taarifa kuu

Paraguay: Santiago Peña wa chama tawala cha Paraguay ashinda uchaguzi wa urais

Nairobi – Santiago Peña wa chama tawala cha Paraguay cha kihafidhina cha Colorado ameshinda uchaguzi wa urais, na kumshinda mpinzani wa mrengo wa kati Efraín Alegre.

Rais mteule wa Paraguay Santiago Peña, wakati wa kampeni zake.
Rais mteule wa Paraguay Santiago Peña, wakati wa kampeni zake. AP - Jorge Saenz
Matangazo ya kibiashara

Bw Peña ambaye ni mwanauchumi, alipata zaidi ya 42% ya kura huku zaidi ya 99% ya kura zikiwa zimehesabiwa. Hii ni zaidi ya alama 15 ya mpinzani wa mrengo wa kati Efraín Alegre, ambaye ametoa hoja ya kubadili kuingua China mkono.

Chama cha Colorado kimetawala ulingo wa kisiasa katika taifa hilo la Amerika Kusini lisilo na bandari kwa zaidi ya miaka 70. Uchaguzi wa urais wa Jumapili uliamuliwa katika duru moja ya upigaji kura.

Akiwahutubia wafuasi wake, Bw Peña, mwenye umri wa 44, alisema: "Asante kwa ushindi huu wa Colorado, asante kwa ushindi huu wa Paraguay."

Vile vile alitoa wito wa kuwepo kwa umoja na maridhiano ya nchi nzima. Uchumi wa Paraguay unatarajiwa kukua kwa zaidi ya 4% mwaka huu, lakini nchi hiyo ina viwango vya juu vya umaskini na ufisadi.

Paraguay kwa sasa ni miongoni mwa nchi 14 pekee ambazo zina uhusiano rasmi wa kidiplomasia na Taiwan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.